Mwanamke
mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Shija Paulo(35),mkazi wa Kijiji
cha Magaga,Kata ya Mbuyuni Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya amejifungua
kiumbe kinachofanana na ng'ombe chenye jinsi ya kiume.
Tukio
hilo limetokea Septemba 16 mwaka huu majira ya saa 11 alfajiri,mwanamke
huyo alipokuwa amepelekwa katika Zahanati ya Mbuyuni kwa ajili ya
kujifungua akiwa na mumewake Bwana Mwigulu Yangula(Makeni) lakini kabla
ya kufika zahanati mwanamke huyo alipatwa na uchungu ndipo alipoomba
msaada kwa Mkunga wa jadi aliyekuwa karibu Bi. Agripina Fredrick
Sikanyika(Namwinje).
Mkunga
huyo alimpokea mwanamke huyo na kujifungua salama huku kiumbe hicho
kikiwa na kichwa na domo mithili ya ndama(mtoto wa ng'ombe) chenye
dalili ya kuota mapembe na manyoya meusi hadi eneo la kifuani ambapo
kutoka hapo kifuani mpaka miguuni alikuwa na umbile la binadamu na jinsi
ya kiume licha ya kutimiza miezi tisha ya kuzaliwa na uzito wa
wastani.
Hali
hiyo ilimtisha sana Mkunga Bi. Sikanyika na kuitwa Bwana Yangula
kushuhudia kiumbe hicho naye alistaajabu kwa yale yaliyotokea.
Hata
hivyo kiumbe hicho kilidumu kwa muda wa masaa matatu na kufariki dunia
na katika uchunguzi wa mwandishi wa habari hii amebaini kuwa hiyo
ilikuwa ni mimba ya nane kwa mwanamke huyo na kila mimba hupata watoto
ambao si riziki.
Tukio
hilo pia lilishuhudiwa na mhudumu wa Kituo cha Afya,kitongoji cha
Magaga Bwana Josephat Alisen Ismail,ambaye naye amesema ameshangazwa na
tukio hilo na kusema hajawahi kukutana na jambo hilo katika taaluma hiyo
ya utabibu.
Wakati
wa tukio hilo Afisa Mtendaji wa Kijiji Bwana Michael Sanziwa hakuwepo
na alipopigiwa simu aliruhusu kiumbe hicho kichukuliwe na mzazi ambapo
maziko yake yalifanyika kandokando ya nyumba ya Bwana Yangula.
Katika
tukio hilo watu wengine wamelihusisha na imani za kishirikina na
wataalamu wa viumbe wamesema kuwa mara nyingi viumbe hivyo huwa haviishi
muda mrefu,lakini hali ya mama aliyejifungua inaendelea vema baada ya
kujifungua.
0 comments:
Post a Comment