Nidhamu ya kazi kushuka na wanafunzi kufanya vibata kwenye mitihani yao.
Na Gabriel Mbwille, Mbeya.
waandishi wa habari mkoani Mbeya wamesema kushukwa kwa
uwajibikaji na utendaji kazi wa watumishi wa idara mbalimbali hapa nchini
kunatokana na mfumo mbovu wa elimu ya sasa hapa nchini.
wameyasema hayo katika mafunzo ya uandishi wa habari kwa njia za mtandao ambayo
yameandaliwa na umoja wa klabu za wa andishi wa nchini (UTPC( na kufanyika katika ukumbi wa
hospitali ya mkoa Mbeya.
wamesema watendaji wa idara mbalimbali wamekuwa wakishindwa
kufanya kazi zao kwa ufanisi kutokana na kukoskana kwa uzoefu, ujuzi na elimu
kwa wakati mmoja.
Mmmoja wa washirii hao SAIDI BENJAMINI amesema hatua ya watendaji kudanganya taarifa kwa viongozi na jamii inatokana na watendaji hao kuwa na elimu bila ya uzoefu na ujuzi wa kazi hali inayowapelekea kutumia tafiti na takwimu za sehemu ambazo haziendani na sehemu husika.
"Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa wa Mbeya ABASI KANDORO akiwa wilayani Mbozi kwa ziara ya kikazi alipewa taarifa kuhusu hali ya kilimo isiyoendana na mazingira halisi ya eneo husika"alisema Saidi.
Naye mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya CHRISTOPHER NYENYEMBE amesema hatua za mabadiliko ya kielimu hapa nchini itabadilika kwa watendaji wakuu wa Serikali kufanya kazi zao kwa kuondokana na mashinikizo ya kisiasa.
"Hivi karibuni Tanzania imengia kwenye mfumo wa usahihishaji wa mitihani ya darasa la saba kwa njia ya mtandao ambapo wanafunzi watakuwa wakiweka vivuli kwenye majibu sahihi badala ya wanafunzi hao kuonesha uwezo walionao kutokana na yale waliyofundishwa ambapo hii inahatarisha zaidi kwa taifa kuwa na wanafunzi wasio na uelewa na elimu kwa sababu ya kuandika majibu yao kwa njia ya kukisia pia huenda ikawa ni njia kubwa ya wanafunzi kupewa majibu ya mtihani kuliko hata tatizo la awali lililojitokeza"alisema Nyenyembe
kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo MAJID MJENWA
amesema mfumo wa Serikali kuangalia zaidi elimu pasipo Ujuzi na uzoefu wa
mazingira umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kutufika hapa tulipo.
Aidha amesema viongozi wa sasa wamekuwa wakishindwa
kutekeleza majukumu yao kutokana na kutojitambua, kujiamini na kuthubutu ikwia
ni pamoja na kufanya kazi zao kwa shinikizo la usiasa badala ya kuangalia namna
ya kutumia jamii.
mwishooooooooo
0 comments:
Post a Comment