KITENDO
cha wanafunzi kukimbia masomo ya sayansi kimechangia kwa kiasi kikubwa
kitengo cha maabara katika hospitali ya mkoa kukosa wataalamu wa
kutosha.
Mratibu
wa Huduma wa Maabara Mkoa wa Mbeya,Dk.Ezikiel Tuya akizungumza na
waandishi wa habari, alisema kitendo cha wanafunzi kukimbia masomo ya
sayansi ni tatizo kubwa katika kitengo cha maabara.
Alisema,
hali hiyo imepelekea kuwepo na upungufu wa wataalamu katika taaluma ya
afya hasa vitengo vya maabara katika hospitali nyingi za hapa nchini.
Hali
hiyo imekuwa ikichangia baadhi ya vifo vya wagonjwa kutokana na
wagonjwa kushindwa kupata vipimo vya ugonjwa kwa wakati na stahiki.
Dk.
Tuya ameiomba serikali kushughulikia hali ya ukosefu wa wataalamu wa
maabara nchini ili kunusuru maisha ya watanzania wanaofariki dunia kwa
kukosa huduma ya vipimo kwa wakati.
Changamoto
nyingine inayoikabili huduma hiyo ni uhaba wa vitendea kazi ambapo
vifaa hivyo vikipatikana vitarahisisha utendaji kazi kwa watumishi.
Hospitali
hiyo ya Mkoa wa Mbeya, ilianza rasmi kutoa huduma za afya mwaka 2001
ambapo mwaka 2002 hospitali hiyo ilipokea vifaa vya maabara vyenye
thamani ya shilingi milioni 200 kutoka kwa wafadhili.
|
0 comments:
Post a Comment