WANANCHI
wametakiwa kuwa makini na watu wanaowambia maneno ya upotoshaji juu ya
uchangiaji wa maoni ya uundwaji wa katiba mpya badala yake wawe na tabia
ya kujitokeza wao wenyewe kwenye mikutano hiyo.
Imeelezwa
kuwa wananchi wengi wamekuwa wavivu kuhudhuria mikutano yenye lengo la
kuleta maendeleo badala yake wanakaa kusikiliza maneno ya uzushi na
kukimbilia kuilaumu serikali.
Rai
hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, RoseMary Senyamule
wakati wa mdahalo wa kuwandaa na kuwahamasisha wananchi kuhusu utoaji
maoni ya katiba, ambapo alisema kuwa upatiakanaji wa katiba mpya yenye
kukidhi mahitaji ya wananchi unategemea mawazo wanananchi wenyewe.
Mdahalo
huo uliandaliwa na mtandao wa mashirika yasio ya kiserikali wilayani
Ileje kwa ufadhili wa shirika la the Foundation Civil Society uliokuwa
na lengo la kuwatayarisha wananchi kabla ya tume ya kukusanya maoni
kufika wilayani humo.
Alisema
kuwa mahudhurio ya wananchi katika mikutano ya kutoa maoni ndio
yanaweza kusadia upatakanaji wa katiba nzuri yenye mawazo shirikishi
kutoka kwa makundi mbalimbali ya jamii ambayo yatapewa nafasi ya kutosha
kuchangia mawazo na maoni yao kuhusu katiba mpya.
“itasikitisha
kama wananchi watashindwa kufika na kushiriki katika mikutano ya tume
ya kukusanya maoni ya katiba, maana hii ni fursa pekee kwa wale ambao
tume hiyo itapita karibu na maeneo yao, na kama wananchi watashindwa
kufanya hivyo badaye wasilaumu kwa yale yote yatakayo kuwa yemingizwa
katika katiba” alisema.
Aliongeza
kuwa Wilaya ya Ileje ni miongoni mwa wilaya ambayo ipo mpakani mwa nchi
ambapo alisisitiza wananchi wasisite kuingiza maoni kuhusu hali ya
mipaka ya nchi yao katika katiba itakayo andaliwa.
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi waliohudhuria mdahalo huo walisema
maandalio ya katiba mpya yazingatie mahitaji ya makundi maalumu na
jinsia pamoja haki ya wananchi kumiliki ardhi yao ili kuondoa migogoro
kati yao na wawekezaji, na kwamba kwa sasa watanzania hawana haki juu ya
ardhi yao kutokana na wawekezaji kupewa nafasi zaidi kuliko wazawa.
Pia
walisema suala la wanawake kunyang’anywa mali na ndugu wa waume zao
mara baada ya kufariki ni kukiuka haki pia ni unyanyasaji wa kijisia
dhidi ya watoto wa marehemu na mke kwa kuwa mke alishiriki kikamilifu
katika utafutaji wa mali hizohivyo suala hilo litambuliwe kikatiba.
|
0 comments:
Post a Comment