
Siku moja
baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuwapokea viongozi
wawili akisema wanatoka Chadema na kumtuhumu Mbunge wa Arusha, Godbless
Lema kuwa anatumia madaraka yake kujinufaisha na mali za umma, mbunge
huyo amejibu akisema: “Kinana amepigwa changa la macho.”Akiwa
Arusha mwishoni mwa wiki Kinana aliwapokea waliokuwa wenyeviti wa
Chadema katika Wilaya ya Monduli, Amani Silanga na wa Ngorongoro,
Revocatus Palapala lakini jana Lema alisema viongozi hao
walikwishatimuliwa Chadema tangu mwaka 2013.Kinana alisema
migogoro ya CCM ndiyo iliyokinufaisha Chadema na Lema akaingia
madarakani, lakini akawataka wananchi kujutia...