Pages

Home » » BAADHI YA WANANCHI TARAFA YA MDANDU WAGOMA KUCHUKUA RUZUKU YA PEMBEJEO YA SERIKALI.

BAADHI YA WANANCHI TARAFA YA MDANDU WAGOMA KUCHUKUA RUZUKU YA PEMBEJEO YA SERIKALI.

 Kaimu katibu tarafa ya Mdandu bwana Benson Wandelage akielezea hali ya mapokeo duni ya pembejeo za ruzuku kwa wananchi wake yalivyo duni.
 Mbolea iliyobaki katika kijiji cha Mdandu aina ya minjingu mazao ambayo baadhi ya wananchi hawana imani nayo kutokana na historia ya kipindi cha nyuma.


Hizo ni mbolea zilizobaki baada ya wakulima kugoma kuzichukua huko mdandu kutokana na serikali kuwataka wakulima kuchukua seti nzima wakati imecheleweshwa.
 
Na.Mwandishi wetu, Njombe.
Wakazi wa tarafa ya Mdandu wilayani Wanging’ombe wamegoma kuchukua mbolea za ruzuku zinazotolewa na serikali kutokana na kufika wakati wakiwa wamekwisha panda mazao.

Katibu tarafa wa kata ya Mdandu Benson Wandelage akizungumza na kituo hiki amesema wakulima wengi tarafani humo wameamua kuacha kuchukua mbolea hizo kutokana na kuja huku wakiwa wamepanda, na kwamba kwa sasa wanahitaji mbolea za kukuzia za urea.

 Bwana Wandelage amesema  tarafa ya Mdandu wananchi wachache tu wamejitokeza kuchukua mbolea hizo lakini wengine hawataki kabisa kuchukua kwa madai kwamba wanahitaji urea tu, lakini sasa kwa utaratibu wa serikali mtu hawezi kuchukua mbolea nyingine wala mbegu bila kuchukua mbolea za Minjingu mazao,

Wakazi wa mkoa wa Njombe licha ya mbolea za ruzuku kuchelewa, lakini wamekuwa wakisuasua kutumia mbolea ya Minjigu Mazao kutokana na kutokuwa na imani nayo baada ya kuitumia mara ya kwanza ikiwa Mijinjingu kuwasababishia kupata mazao duni.

Ameeleza kuwa kwa sasa mkuu wa wilaya hiyo Esterina Kilasi amewaagiza wataalamu wa ugani kuwa na shamba la mfano kwa ajili yakutolea elimu kwa wakulima katika maeneo yao ikiwemo kufanya majaribio ya vitendo kwa kutumia mbolea hizo za minjingu mazao.

Hata hivyo wataalam wa kilimo wamekuwa wakijaribu kutoa elimu kwa wakulima juu ya mbolea hiyo, juhudi ambazo bado hazijazaa matunda ya kutosha katika kubadilisha fikra za wakulima za kujenga imani na mbolea hiyo.

Mbolea ya minjingu mazao awali ilidaiwa kutokuwa na madini ya nitrogen, lakini licha ya kuboreshwa kwa kuwekewa madini hayo wananchi wameendelea na msimamo wa kutokuwa na imani nayo, hali ambayo imepelekea ugumu katika ugawaji wa mbolea za ruzuku mkoani hapa baada ya serikali kutoa mwongozo kwamba kila mlengwa wa vocha ya pembejeo lazima achukue mifuko miwili ya minjingu mazao.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger