Mwanamke
mmoja nchini Marekani amepandishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwaua
watoto wawili kwa kuwachoma visu, katika kile kinachoaminika ni kuonesha
hasira zake kwa mumewe.
Mwanamke
huyo Elzbieta Plackowska mwenye umri wa miaka 40 na mhamiaji kutoka
Poland, anatuhumiwa kumuua mtoto wake mwenyewe wa kiume Justin mwenye
miaka 7, na mtoto wa kike aliyekuwa akimlea mwenye umri wa miaka mitano.
Mamlaka za jimbo la Illinouis zinasema kwamba Justin alipigwa visu mara 100.
Mkuu
wa polisi wa eneo hilo amesema kwamba hilo ni tukio baya kabisa
kulishuhudia tangu aanze kazi ya upolisi miongo mitatu iliyopita.
Mwendesha
mashitaka amesema kwamba Plackowska alifanya mauaji hayo akiwa na
hasira dhidi ya mume wake, dereva wa gari kubwa, na ambaye mara nyingi
huwa hayupo nyumbani.
0 comments:
Post a Comment