Pages

Home » » MKUU WA MKOA WA NJOMBE AAGIZA KUUNDWA HARAKA KWA BODI YA MAJI MRADI WA WANGING'OMBE NA TOVE MTWANGO.

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AAGIZA KUUNDWA HARAKA KWA BODI YA MAJI MRADI WA WANGING'OMBE NA TOVE MTWANGO.


 Mkuu wa Mkoa wa Njombe akipata maelekezo ya kitaalamu eneo la chanzo cha maji hayo huko masaulwa.
 Hali ya chanzo cha maji kilivyo kwa sasa licha ya kuwa ni msimu wa masika.
 Mhandisi wa maji wa mradi wa kitaifa wa Wanging'ombe bwana Bakari Mbinga akipokea maelekezo kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Capt.Mstaafu Asseri Msangi juu ya uendeshaji wa mradi huo.

 Mkuu wa mkoa wa Njombe akizungumza na kutoa maagizo kwa katibu tawala mkoa wa Njombe Bi.Mgeni Baruani kufuatilia uundaji wa bodi ya mradi wa maji wa wanging'ombe na Mradi wa Tove Mtwango.[katika ni meneja wa mradi wa maji wa Kitaifa wa Wanging'ombe Eng. Bakari Mbinga].


 Matenki chanzo mradi wa maji wa Kitaifa wa Wanging'ombe yakiwa yamekauka kutokana na kukatika miundombinu yake.

 hiki ni chanzo cha maji hayo kilichopo kijiji cha Masaulwa wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe.

Na.Mwandishi wetu.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kepten Mstaafu Aseri Msangi, amemwagiza katibu tawala wa mkoa Njombe Mgeni Baruani kufuatilia utendaji kazi wa mradi wa taifa wa Maji wa Mbukwa uliopo wilayani  Wanging’ombe pamoja na ule wa Tove Mtwango uliopo wilayani Njombe ili kuangalia namna inavyotekeleza majukumu yake kwa wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa agizo hilo baada ya kutembelea chanzo cha mradi wa maji wa Mbukwa, na kushtushwa na taarifa ya Meneja wa mradi huo Mhandisi Bakari Mbinga, kwamba kwa sasa anafanya kazi bila kutoa taarifa ya utendaji kazi kwenye bodi kutokana na kutokuwa na bodi ya maji, licha ya kuwa anapaswa kuwajibika kwenye bodi hiyo  na kwamba kwa sasa  anawasilisha taarifa zake za kazi katika wizara ya maji pekee.

Meneja wa mradi huo wa maji Wanging’ombe taifa Kwa sasa amesema anapeleka taarifa wizarani pekee kwa kuwa bado hakuna  bodi ambayo anatakiwa  kutoa taarifa za mradi .

Baada ya kupokea taarifa za mradi huo kutoka kwa meneja, mkuu huyo wa mkoa alimwagiza katibu tawala wa mkoa wa Njombe Mgeni Baruani kufuatilia mradi huo pamoja na ule wa Tove Mtwango ili kuangalia namna inavyofanya kazi na kuwataka mameneja wa miradi hiyo kutoa taarifa za utendaji wao katika halmashauri husika, na kuunda bodi haraka iwezekanavyo.

Kutokana na hali hiyo aliomba ufafanuzi juu ya mikakati ya kukarabati miundombinu hiyo kutoka kwa meneja wa mradi, ambaye alisema walishaandika kuomba sh. 99 bilioni ili kujenga upya miundombinu hiyo kwa ajili ya kuwezesha maji kuhifadhiwa kwenye matenki.

Katika hatua nyingine Msangi aliwataka wahandisi wa miradi ya maji mkoani Njombe kuweka mita za maji kwa watu binafsi wanaowaunganishia huduma ya maji ili kuepuka upotevu na utumiaji wa maji ovyo.

“Katibu tawala fuatilia hii miradi jinsi inavyofanya kazi, na uhakikishe wanaunda bodi haraka kwa sababu haiwezekani mtu afanye kazi kwa uhuru anavyojiamria yeye bila mtu wa kumdhibiti,” alisema Msangi na Kuongeza.

“Mameneja wa miradi hii lazima mtoe taarifa za utendaji kazi wenu kwa halmashauri, maana haiwezekani taarifa zipelekwe wizarani Dar Es Salaam pekee wakati wanaokunywa maji haya ni watu wangu, na ndio maana serikali ikaamua kusogeza mamlaka kwenye halmashauri. ”  

Alisema inashangaza kuona hata mradi wa Tove Mtwango mpaka sasa hauna bodi ya maji tangu uzinduliwe na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2011.   

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alishangaa kuona matenki ya maji ya mradi huo hayafanyi kazi kutokana na  kuvunjika kwa miundombinu, na hivyo kulazimika maji kuunganishwa moja kwa moja mpaka kwa watumiaji bila kuhifadhiwa kwenye matenki na kutibiwa, jambo ambalo alisema ni hatari kwa afya za wananchi kutokana na kunywa maji ambayo si safi na salama.

Kutokana na hali hiyo aliomba ufafanuzi juu ya mikakati ya kukarabati miundombinu hiyo kutoka kwa meneja wa mradi, ambaye alisema walishaandika kuomba sh. 99 bilioni ili kujenga upya miundombinu hiyo kwa ajili ya kuwezesha maji kuhifadhiwa kwenye matenki.

Katika hatua nyingine Msangi aliwataka wahandisi wa miradi ya maji mkoani Njombe kuweka mita za maji kwa watu binafsi wanaowaunganishia huduma ya maji ili kuepuka upotevu na utumiaji wa maji ovyo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger