Pages

Home » » YANGA KUCHEZA NA ARMINIA BIELEFELD

YANGA KUCHEZA NA ARMINIA BIELEFELD



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Timu ya Young Africans Sports  Club yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam nchini Tanzania siku ya jumamosi itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Arminia Bielefeld ya kutoka nchini Ujerumani, mchezo utakaofanyika katika mji wa Antalya.
Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa pekee ya kuweza kujipima uwezo dhidi ya timu hiyo ya Ujerumani ambayo pia imekuja kambi y amafunzo kujiandaa na mzunguko wa ligi daraja la pili nchini Ujerumani.
Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Armini Bielefeld ambayo inawachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
Unajua tun siku sita (5) tangu tufike hapa mjini Antalya Uturuki na tumeshafanya mazoezi kwa siku  nne (4) hivo fursa ya kupata mchezo wa kirafiki ni nzuri sana kwetu kwani itanipa nafasi ya kuona wachezaji wangu wameshayashika kwa kiasi gani mafunzo yangu alisema 'Brandts'
Arminia Bielefeld  imeshawasili mjini Antalya kwa ajili ya kambi yake ya mafunzo na hivyo kwao pia ni fursa nzuri ya kuweza kujipima uwezo na timu ya Young Africans ambao ni mabingwa mara 23 katika ligi kuu ya Tanzania.
Leo asubuhi Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa siku ya jumamosi mjini Antalya.
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger