MJUMBE wa Kamati ya Utendaji wa Jumuiya ya wanawake Tanzania(Uwt) Mkoani
Ruvuma Amina Chimata (55) mkazi wa mjini Tunduru amefariki dunia akiwa
chooni kwenye nyumba ya kulala wageni ya Tulia iliyopo karibu na kituo
cha mabasi Songea
Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na Katibu
wa Chama cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Ruvuma Verena Shumbusho zimesema
kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa za asubuhi wakati Chimata
alipokuwa akijiandaa kwenda kuhudhuria kikao cha Kamati ya Siasa ya
chama hicho mkoa
Shumbusho alifafanua kuwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa mkoa
walikuwa tayari wameshafika kwenye eneo la Ccm Mkoa kwa ajiri ya kuanza
kikao hicho na ghafla mmoja wa wajumbe alipigiwa simu toka kwa muhudumu
wa nyumba ya kulala wageni ya Tulia kuwa aende haraka kwenye nyumba hiyo
kwani Chimata tangu alivyoingia bafuni na baadae aliingia chooni kwenda
kujisaidi hajatoka kwa muda mrefu
Alifafanua zaidi kuwa baada ya mjumbe huyo kupokea taarifa hiyo
aliwasiliana na viongozi wa Ccm Mkoa kisha walikwenda kwenye eneo la
tukio ambako walikuta mlango wa choo hicho ukiwa umevunjwa na Chimata
akiwa amelala kwenye sakafu ya choo hicho huku Polisi wakiwa tayari
wameshaanza kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo ambapo mwili wa
Chimata ulichukuliwa na kupelekwa kwenye Hospital ya Serikali ya Mkoa wa
Songea kwa ajiri ya uchunguzi zaidi ambako ilithibitika kuwa Chimata
alikuwa tayari amefariki dunia kwa ugonjwa wa shinikizo la damu na
kisukari
Alisema kuwa kutokana hilo kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa na badala
yake wajumbe walikutana wakiwa na huzuni ili kuweza kupanga kuusafirisha
mwili wa marehemu kwa mazishi
Kwa upande wake Katibu wa Uwt mkoa wa Ruvuma Mariam Yusuph alipoulizwa
kuhusiana na tukio hilo alisema kuwa Uwt Mkoa wa Ruvuma na Taifa
kiujumla imepata pigo kubwa sana kutokana na kuondokewa na kiongozi huyo
ambaye alikuwa ni msaada mkubwa sana kwenye jumuiya na chama kwa ujumla
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa lilitokea agosti 15 mwaka huu
majira ya saa 4:30 asubuhi katika nyumba ya kulala wageni ya Tulia na
uchunguzi wa awali umebainisha kuwa Chimata katika uahi wake alikuwa
anasumbuliwa na magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu kwani baada ya
tukio hilo kutokea alikutwa akiwa amehifadhi dawa ya magonjwa hayo
kwenye mfuko wake
NEW VIDEO:- CHRIS BEE - SIENDI MBALI
6 years ago
0 comments:
Post a Comment