Naibu
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mheshimiwa ADAM MALIMA ametangaza
kuwa siku za watu wenye tabia ya kuchakachua Mbolea za Kilimo kwa
wakulima kwa kuchanganya Simenti na Chumvi katika Mbolea hizo
zinahesabika.
Mheshimiwa
MALIMA ametangaza kauli hiyo leo jijini Dar es salam wakati akizungumza
katika Kipindi cha Hello Tanzania kinachorushwa na Kituo cha Uhuru FM
kila siku Asubuhi, huku akisema watu hao watafikishwa Mahakamani ili iwe
fundisho kwa wengine.
Naibu
Waziri huyo amesema kuhesabika kwa siku za watu hao inatokana na mpango
wa serikali wa kumpa mamlaka zaidi Mthibiti wa Mbolea Nchini kuwakamata
na kuwakuchukuliwa hatua kali za kisheria watu hao wanaorudisha nyuma
maendeleo ya mkulima nchini.
Kazi
ya Mthibiti huyo wa Mbolea Nchini ni kusimamia ipasavyo masuala yote ya
mbolea na kuishauri serikali njia za kukomesha mtandao unaotumiwa na
watu wasiowatakia mafanikio wakulima kwa kuwachakachulia Mbolea za mazao
kwa manufaa yao binafsi.
Kuhusu
suala la malipo ya Korosho kwa wakulima wa Tunduru, Rufiji na Mkurunga,
Mheshimiwa MALIMA amewakata kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea
kufuatilia malipo hayo ambapo katika Wilaya ya Mkuranga tayari pesa za
wakulima zimeshapelekwa na anashangaa ni kwa nini hawajalipwa bado.
0 comments:
Post a Comment