JE UNAMPENDA NANI: Carnavalesca, Bossa Nova au Brazuca??
Uchaguzi huu wako ni wazo la Kampuni ya
Adidas ambayo ndio watengenezaji wa Vifaa rasmi kwa ajili ya Fainali za
Kombe la Dunia za Mwaka 2014 na wao watatengeneza Mpira maalum
utakaochezewa kwenye Fainali hizo na sasa wapo kwenye mchakato wa kuupa
Jina Mpira huo maalum.
Adidas wamependekeza Majina matatu,
Carnavalesca, Bossa Nova au Brazuca, yote ni Majina, maneno ya Kireno,
na yote yana mizizi ya Kike, na hilo linalingana na falsafa ya Brazil
kuwa Mpira ni kama Mwanamke, inabidi uubembeleze na kuutunza.
Carnavalesca ni neno linalomwelezea Mtu
anaetaka kushiriki au anaeshiriki kwenye zile sherehe asilia za huko
Brazil ‘Carnival’ ambazo Watu hupita Mitaani wakipiga ngoma, kucheza na
kuimba mithili ya ‘Mdundiko’ wa Bongo.
Jina la Bossa Nova linahusu Muziki wa
Jazi, Samba, ambao uliibuka huko Rio de Janeiro na kutapakaa kote
Duniani kuanzia Miaka ya 1950 na 1960.
Brazuca ni neno la mtaani na la utani
likimaanisha Wazalendo wa Brazil na hili limewekwa ili kuonyesha
msisitizo wa asili ya Raia wa Brazil.
Huu mtindo wa kutoa Majina kwa Mipira
inayotumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia ulianza kwenye Fainali za
huko Mexico Mwaka 1970 na Mpira wake ukaitwa Telstar.
Majina mengine ya Mipira ambayo
yatakumbukwa ni Tango wa Fainali za Argentina Mwaka 1978, Azteca wa
Mexico 1986 na Jabulani wa Afrika Kusini Mwaka 2010
0 comments:
Post a Comment