RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzanzania Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kuwa na ziara ya siku nne mkoani Kilimanjaro kuanzia tarehe 28-31 Oktoba mwaka huu.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari mkoani humo juu ya ujio huo mapema leo, Mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amesema katika ziara hiyo atazindua miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi katika
mikutano ya hadhara. Gama amesema katika ziara hiyo Rais ataweza kutembelea
halmashauri za wilaya tano za mkoa wa Kilimanjaro ambapo ni Same,Mwanga,
Rombo,Hai Moshi Manispaa. Mkuu huyo wa mkoa amesema katika wilaya ya Same
Rais atapata fursa ya kuzungumza na
wananchi,kuzindua kiwanda cha tangawizi kilichojengwa kwa nguvu za raia ikiwa
ni pamoja na kutembelea wahanga 8 walioathirika katika maporomoko ya udongo na
kuzindua nyumba alizoahidi kuwajengea wahanga hao. Amesema katika wilaya ya
Mwanga atazindua mabweni ya shule ya wasichana ya Asha Rose Migiro na kuweka
jiwe la misingi ambapo katika wilaya ya Rombo atazindua mradi wa barabara ya
Mkuu/Tarakea.
Aidha Gama amesema kusema katika wilaya ya Hai
atapata fursa ya kuweka jiwe la msingi katika Sadala/Masama na katika Manispaa
ya Moshi ataweza kuzindua jengo la Mkaguzi Mkuu wa serikali (CAG).
0 comments:
Post a Comment