Pages

Home » » KIONGOZI WA DINI ATAKAYE BAINIKA KUPOTOSHA UMMA KUKIONA MBEYA

KIONGOZI WA DINI ATAKAYE BAINIKA KUPOTOSHA UMMA KUKIONA MBEYA

Serikali mkoani Mbeya imesema imeanza kuchukuwa hatua dhidi ya mtu anayesambaza ujumbe mfupi wa maandishi wenye lengo la kuleta uhasama ndani ya jamii.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro katika kikao chake na waandishi wa habari mkoani hapa, kikao kilichoudhuriwa pia na viongozi wa kidini kutoka pande mbili za waislam na wakristo.
Katika mazungumzo yake Kandoro amesikitishwa na tabia iliyofanywa na mtu aliyebuni maneno na kuyatuma kwa watu kuhusu Malawi kutupa Mabomu ya kurushwa kwa mikono katika mipaka ya Tanzania.
Aidha amesema kuwa kamwe Jeshi haliwezi kuzungumza na wananchi wake kupitia sms hivyo ujumbe huo ni batili na umelenga kuchafua amani iliyopo hapa nchini.
Mbwille Media nayo ilitumiwa ujumbe huo na ulikuwa ukisema kama ifuatavyo "HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE.MTANZANIA YEYOTE :Kaa makini usiokote kitu chochote ambacho unamashaka nacho kuna mabomu yametupwa kutoka nchi jirani ya Malawi zaidi ya 30 zenye uzito usiopungua tani 100.Hivi unapoona kitu kama chupa ya chai kinarangi ya fedha "Usikiguse"piga simu namba 0777756000042.SMS HII TUMA KWA WATU UWEZAVYO imetolewa na JWTZ/LSL5CAMRM,Asante kwa kutumia VODOCOM"huo ndio ujumbe ulikanushwa na Serikali.

Wakati huohuo Viongozi wa kidini mkoani Mbeya kwa pamoja wameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka dhidi ya muumini ama kiongozi yeyote atakayebainika kutoa lugha zenye kuhatarisha amani katika madhabahu ili kudhibiti hatari za uvunjifu wa amani zinazoweza kujitokeza.

katika kikao hicho walikuwepo viongozi wa Kiislam na kikristo ambao wote walienda mbali zaidi wakisema kuwa kiongozi wa dini ambaye anahamasisha vurugu hana nia ya kweli hivyo haiba budi kuchukuliwa hatua za kisheria kwa haraka.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger