Pages

Home » » Maambukizi Ya Ukimwi Kwa Wanawake Wanaofanya Biashara Ya Ngono Yaongezeka Dar

Maambukizi Ya Ukimwi Kwa Wanawake Wanaofanya Biashara Ya Ngono Yaongezeka Dar

 

Kaimu mkurugenzi wa Idara ya Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Bw. Elias Chanamo (katikati) akitoa ripoti kwa waandishi wa habari juu ya utafiti kuhusu maambukizi ya Ukimwi miongoni mwa wanawake wanaofanya biashara ya ngono jijini Dar es Salaam jana. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.  

Na Aron Msigwa – MAELEZO, Dar es Salaam 

WATANZANIA wametakiwa kujiepusha na vitendo vinavyochangia kueneza Ugonjwa wa Ukimwi kufuatia matokeo ya utafiti wa kibiolojia na kitabia uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi ( NACP) kuonyesha kuwa maambukizo ya ugonjwa huo kwa wanawake wanaofanya biashara ya ngono jijini Dar es Salaam yapo juu kwa asilimia 31.4. 
Kauli hiyo imetilewa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Elias Chinamo wakati akifungua mkutano wa kuwasilisha ripoti ya utafiti ya mwaka 2009/2010 kuhusu maambukizi ya Ukimwi miongoni mwa wanawake wanaofanya biashara ya ngono jijini Dar es Salaam. 
Amesema kiwango hicho cha maambukizi kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo kinaenda sambamba na ongezeko la magonjwa mengine yakiwemo Kaswende ambayo ni 2.0%, Gonorea 10.5%, Pangusa 6.3% na Trakoma ya via vya uzazi ambayo ni 15% na kukifanya kiwango hicho kufikia asilimia 31.4 ikilinganishwa na asilimia 10.4 ya kiwango cha maambukizi kwa wanawake wote wa mkoa huo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger