ameanza mchakato wa kutusua kimataifa na sasa yupo mbioni kuhamishia makazi yake nchini Zambia.
Mwingizaji huyu ambaye pia ni Director wa movie chini ya kampuni yake ya A Jerusalem Company siku ya leo amechonga na BK Cop kuhusiana na kupata shavu kutoka kwa waandaaji wa filamu nchini humo na tayari wameshakamilisha taratibu zote za yeye kwenda huko kwa ajili ya kufanya kazi za sanaa.
Kuhusiana kitu ambacho kinamfanya mpaka sasa yupo nchini mkali huyu wa filamu kama “DJ Ben” na sasa “Ukurasa Mpya” alifunguka kwa kusema “Kinachonikwamisha kwa sasa ni mkataba nilionao hapa Bongo, nikimaliza basi nitakwenda huko kwa sababu masilahi ni makubwa zaidi ya hapa nyumbani,”
“Kimsingi nitahamia huko na familia yangu kabisa, pia nitaongozana na wasanii wachache. Shughuli zote za filamu nitakuwa nazifanyia huko. Kiukweli jamaa wamenipa dau kubwa sana, ni mara tatu ya fedha ninayopata (kwa kila filamu) hapa nchini.” - JB.
0 comments:
Post a Comment