SINGIDA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana,
Jumapili, Novemba 4, 2012, ameweka jiwe la msingi kwenye mradi mkubwa wa maji
unaolenga kumaliza tatizo la maji mjini Singida.
Rais Kikwete ameweka jiwe la
msingi katika sherehe ya kufana iliyofanyika katika eneo la Mradi la Mwankoko,
nje ya mji wa Singida, mara baada ya kuwasili Mkoani Singida kuanza ziara ya
siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo akitokea Mkoani Manyara
ambako alifanya shughuli hizo hizo kwa siku mbili pia.
Mradi huo ulioanza kujengwa
Novemba 2, mwaka 2009, umekamilika kwa kiasi cha asilimia 80 na unatarajiwa
kukamilika ifikapo Desemba 31, mwaka huu wa 2012.
Kwa mujibu wa maelezo ya
wasimamizi wa Mradi wa SUWASA, Mradi huo unagharimu dola za Marekani milioni
19.7 sawa na Sh.bilioni 31.126.
Kati ya fedha hizo, Serikali ya
Tanzania imetoa dola za Marekani milioni 10.42 sawa na Sh. 16, 463,600,000,
Benki ya Maendeleo ya Nchi za Kiarabu (BADEA) imetoa dola za Marekani milioni
4.57 sawa na Sh. 7,220,600,000 na Mfuko wa OPEC kwa Maendeleo ya Kimataifa wa
OFID umetoa dola za Marekani milioni 4.7 sawa na Sh. 7,426,000,000.
Mradi huo unaotekelezwa na
Kampuni ya Spencon Services Limited unatarajiwa kutoa lita 17,208,000 kwa siku
kutokana na visiwa viwili vilivyoko Mwankoko vyenye uwezo wa kuzalisha lita
292,000 kwa saa na visima viwili vilivyoko eneo la Irao vyenye uwezo wa
kuzalisha tani 425,000.
Mradi huo unatarajiwa kutoa
huduma kwa jumla ya wateja 3,500 kati yao 2,500 katika awamu ya kwanza na
wengine 1,000 katika awamu ya pili.
Mradi huo utaongeza upatikanaji
wa maji kwa karibu kiasi cha asilimia 100 kwa wakazi wa mji wa Singida na
utaongeza muda wa kupatikana maji kutoka saa tano za sasa kwa siku hadi saa 24
kwa siku.
0 comments:
Post a Comment