Pele
alisema wachezaji wengi waliocheza jana wana viwango vya kucheza Ulaya, ingawa
amemsifia zaidi Niyonzima, kwamba anastahili kabisa kucheza moja ya klabu kubwa
hata Ulaya.
Pele
ambaye akiwa Chamazi amejionea mambo mbalimbali, ikiwemo mradi wa maendeleo ya
soka ya vijana, Academy aliousifia sana na kusema utaleta matunda makubwa
Tanzania baadaye, alikuwepo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana Yanga ikiilaza
Azam 2-0.
Akiizungumzia
Azam kwa ujumla, amesema miaka kadhaa ijayo itakuwa klabu kubwa yenye hadhi
sawa na Manchester United ya England kutokana na uwekezaji wake mzuri.
Amesema
akademi ya Azam ni nzuri na bora kuliko hata akademi yake. Pele pia ameishauri
Azam kuachana na desturi ya kuchukua wachezaji wa nje ya nchi, kwani kama
wataitumia vizuri akademi yao kwa kusaka vipaji zaidi nchi mzima, mbele ya watu
zaidi ya Milioni 40 watapata wachezaji bora.
Pele
ambaye ameahidi kuanzisha ushirikiano wa akademi yake na ya Azam, baada ya
kuombwa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga.
Akiizungumzia
Ligi Kuu ya Tanzania baada ya kuona mechi ya Yanga na Azam, Pele alisema ina
ubora sawa na ligi nyingine kubwa Afrika na akasema sasa kinachotakiwa ni
kuongeza maboresho.
Kuhusu
wachezaji, kulingana na alivyoona mechi ya jana, Pele alisema kwamba wana uwezo
sawa na wachezaji wengi duniani na ili watimize ndoto za kucheza Ulaya,
wanatakiwa kuongeza juhudi.
Awali ya
hapo, mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ghana na klabu ya Olympique
Marseille ya Ufaransa, aliwaambia wachezaji chipukizi wa Tanzania kwamba,
hakuna njia ya mkato katika kutafuta mafanikio na kuwataka kufanya jitihada ili
watimize ndoto zao, ikiwa ni pamoja na Serengeti Boys kuhakikisha inafuzu
kucheza fainali za Afrika mwakani.
Pele,
ambaye aliiongoza Marseille kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 1992 akifunga moja ya
mabao dhidi ya AC Milan ya Italia, alisema hayo Jana asubuhi wakati
alipotembelea Kiti cha ufundi cha Karume kushuhudia programu ya mazoezi ya
vijana wadogo inayofanyika kila misho wa wiki kwenye Uwanja wa Karume ambako
watoto wa kuanzia umri wa miaka sita hadi 17 hufundishwa mbinu za kusakata
soka.
0 comments:
Post a Comment