Vijana wa Manispaa ya Iringa wakifukua makaburi ya Igumbilo kupisha mradi wa umeme Iringa- Shinyanga |
Vijana wakitazama mabaki ya mwili wa binadamu baada ya kuchimba moja kati ya kaburi eneo hilo la Igumbilo |
Hili ni eneo jipya ambalo limechimbwa makaburi zaidi ya 100 |
Vijana wengi wamejitokeza kuifanya kazi hi |
Mmiliki wa mtandao huu mzee wa Matukio daima (kulia) akimtazama mmoja kati ya vijana ambao wanafanya kazi ya kufukua makaburi eneo la Igumbilo mjini Iringa ,kaburi moja wanafukua kwa shilingi 70,000 |
Mmoja kati ya vijana akichimba kaburi peke yake |
Na, Matukio Daima, Iringa
BAADHI
ya vijana wasio na ajira katika Manispaa ya Iringa mkoani Iringa
leo wamejitokeza kwa wigi katika eneo la Igumbilo mjini Iringa
kufukua mabaki ya miili ya watu waliozikwa katika makaburi ya
Igumbilo ili kupisha mradi mkubwa wa umeme unaotarajiwa kupitia
eneo hilo kuelekea mkoa wa Shinyanga .
Mwandishi
wa habari hizi alishuhudia vijana zaidi ya 50 ambao wamekuwa
wakishinda vijiweni wakigombea kufukua makaburi ya zamani na kutoa
mabaki ya miili hiyo na kwenda kuizika katika eneo jipya ambalo
limetengwa na uongozi wa serikali ya kijiji cha Igumbilo ambalo ni
eneo la jirani na eneo hilo la awali.
Wakizungumza
kwa sharti ya kutotaja majina yao vijana hao ambao baadhi yao ni
wanafunzi wa vyuo vya ufundi na shule za
sekondari mjini Iringa wamedai kuwa kati ya shughuli ambazo
zimeweza kuwapatia fedha za haraka zaidi ni pamoja na mradi huo wa
umeme ambao umetoa ajira kwa vijana wengi zaidi.
Vijana
hao walisema kuwa wamekuwa wakilipwa kati ya shilingi 40,000 na
shilingi 70,000 kwa siku kwa kuchimba na kufukua kaburi moja hivyo
kutokana na mradi huo wa umeme wameweza kunufaika zaidi.
"Kweli
huu mradi umetusaidia sana vijana tusio na kazi ya kufanya kwani
hapa leo ukichimba kaburi moja unalipwa shilingi 40,000 wakati
mfukuaji wa kaburi na kuzika ni shilingi 70,000 kwa siku....hadi
sasa vijana tunagombea kuchimba na kufukua makaburi haya "
Hata
hivyo vijana hao walisema kuwa wamekuwa wakiifanya kazi hiyo
kwa hofu kubwa kutokana na kuwepo kwa taarifa za imani za
kishirikina kuwa badhi ya maeneo kama hayo ya makaburi huwa kunatokea
mauza uza wakati wa kuhamisha makaburi japo katika eneo hilo hadi
sasa hawajakutana na mauza uza yoyote.
Afisa
afya wa Manispaa ya Iringa Sevelin Tarimo ambae amekuwa akisimamia
shughuli hizo za ufukuaji na uzikaji wa mabaki ya miili hiyo alisema
kuwa taratibu zote za mazishi pamoja na zile za haki ya binadamu
katika kuhifadhiwa zimekuwa zikifuatwa katika
zoezi hilo.
Tarimo
alisema kuwa ndugu wa marehemu waliozikwa katika maeneo hayo wote
wamelipwa fidia na kuruhusu makaburi hayo kuhamishwa na kuwa hadi
sasa zoezi kama hilo limefanyika eneo la Nduli ,Kigonzile na eneo
hilo la Igumbilo.
0 comments:
Post a Comment