Msanii
wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikwa na wasanii wenzake mara
baada ya kuanguka jukwaani juzi ndani ya uwanja wa Sheikh Amri katika
tamasha la wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wale wa filamu.
Msanii huyo akitafakari kwa kina mara baada ya kuanguka chini ya jukwaa huku wenzake wakimpa pole.
Msanii
wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikiliwa na wenzake
wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka alipopewa nafai ya
kuwasalimia mashabiki wake
(Picha na mdau wa Fullshangwe Mahmoud Ahmad-Arusha)
………………………………………………………………………….
Mahmoud Ahmad,Arusha
HALI ya msanii wa filamu
nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha
mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani mara baada ya
kuishiwa na nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki
waliofurika kumtizama.
Tukio hilo lilitokea juzi
jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi
kipya lililofanyika ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid
wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
Mara baada ya msanii huyo
kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia
mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno
moja tu”ahhh” na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua
chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake.
Hatahivyo,wasanii hao
walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya
muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa
kupumzika zaidi.
Akihojiwa na gazeti hili muda
mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema
kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji
matibabu zaidi.
”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
Hatahivyo,baadhi ya mashabiki
waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali ya
msanii huyo huku wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya wasanii wa
filamu nchini walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba wanamtumia
ili wapate pesa ilhali mwenzao ni mgonjwa.
Wakihojiwa kwa nyakati tofauti
mashabiki hao kwa jazba walisema kwamba msanii huyo alipaswa kupewa muda
mwingi wa kupumzika kuliko kuambatana na wenzake mikoani kwani hali
hiyo inamchosha zaidi.
“Hawa watu wa Bongo movie ni
watu wa ajabu sana huyu mtu anaumwa sana sisi tunashangaa wanaambatana
na mtu mgonjwa mikoani wampe muda apumzike na si kumtumia kwa kupata
pesa”alisikika shabiki mmoja akiongea kwa jazba
0 comments:
Post a Comment