Baadhi
ya Viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walioalikwa
katika sherehe za Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
(SUZA) zilizofanyika leo katika kampasi ya Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja. .
Wahitimu
wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ngazi ya Stashahada ya
Lugha na Elimu, wakati walipokuwa wakitunukiwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) pia Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), katika sherehe za
mahafali ya nane ya Chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya
Tunguu.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ,akitoa
zawadi kwa mwanafunzi bora katika fani ya Cheti cha Teknolojia ya
Habari,(IT) kwa Lukuman Mohamed Bachu,katika sherehe za Mahafali ya
nane ya Suza,huko katika kampasi ya Tunguu leo.
Baadhi ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha
Zanzibar (SUZA) ,akitoa hutuba yake baada ya kuwatunuku Shahada,katika
sherehe za Mahafali ya nane ya chuo zilizofanyika huko katika kampasi
ya Tunguu
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
0 comments:
Post a Comment