Pages

Home » » Mchakato wa ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa dar es Salaam waanza...

Mchakato wa ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa dar es Salaam waanza...

 
KAMPUNI mbalimbali zimejitokeza kuomba tenda ya ujenzi wa jengo la abiria la ‘Terminal three’ katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inatokana na kuhamishwa kwa wakazi 1,230 katika eneo hilo ambalo mamlaka husika iliwalipa jumla ya Sh18 bilioni na kuwahamishia katika maeneo ya Pugu Mwakanga na Kinyamwezi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini(TAA), Mchengela Hanga alisema, tayari wizara ya uchukuzi imeshaanza kupokea maombi hayo.

“Tumefungua tenda hiyo ili kuhakikisha tunapata kampuni ambayo itakuwa na uwezo mzuri wa kufanya kazi hiyo, halafu mimi siwezi kutoa taarifa zaidi ya hapo,” alisema Hanga.

Taarifa kutoka Wizara ya Uchukuzi inaeleza kuwa, wizara hiyo kupitia TAA ilitenga fedha za kufanyia upembuzi yakinifu wa jengo hilo kwa lengo la kutambua mahitaji halisi katika ujenzi huo.
“Kwa kuzingatia utaratibu na sheria ya kushirikiana na sekta binafsi,tumeshakamilisha hatua za awali na kuwakilisha mahitaji ya mradi huo kwenye ngazi husika za Serikali”ilinukuu sehemu ya taarifa hiyo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger