Chama
cha Soka cha Zambia (Faz) kimesema kinakusudia kuikabili Fifa ili iweze
kuitambua kazi iliyofanywa na mshambuliaji Godfrey Chitalu wa nchi hiyo
kwa kufunga magoli 107 mwaka 1972.
Hatua
hiyo imefuatia Lionel Messi kutangazwa kuvunja rekodi ya Mjerumani Gerd
Mueller ya kufunga magoli 85, ambapo kwa sasa mwanasoka huyo wa
Argentina ana magoli 88 kufikia mwaka huu 2012.
Msemaji
wa chama cha Soka cha Zambia (Faz) Eric Mwanza amekaririwa akiiambia
BBC Michezo kuwa, chama hicho kinazo rekodi za kudhibitisha kazi ya
Chitalu, hivyo kutaka mchango wake katika soka utambuliwe kimataifa.
0 comments:
Post a Comment