Akizungumza Ikulu kwa masikitiko makubwa huku akitoa machozi, Rais Obama alisema kitendo cha kuwaua wanafunzo hao ni cha kinyama na hakiwezi kuvumiliwa hivyo ni vema watu wote waliohusika katika shambulio hilo wakakamatwa na kuchukulia hatu kubwa za kisheria.
Uchunguzi wa awali ubebaini kuwa mtu aliyekuwa anafyatua risasi zilizo sababisha vifo hivyo ni Adam Lanza ambaye naye aliweza kufariki katika sakata hilo.
"nimeviagiza vitengo vya usalama kuhakikisha kuwa vinatafuta kila uwezekano wa kuwachukulia hatua wahusika, na kutafuta chanzo cha uvamizi huo, mana haiwezekani mtu aanze kuvamia eneo bila sababu,"alisema Rais Obama.
Taarifa imeeleza kuwa wanafunzi 18 waliweza kufariki papo hapo wakati wengine wawili walikufa wakiwa wanapatiwa huduma ya kwanza hospitalini, pia watu wazima sita nao wamekufa akiwemo mtu mmoja anayedhaniwa kuwa alikuw miongoni mwa wafyatua risasi
Hili ni tukio la pili linalofanana na lile lililotokea mwaka 2007 katika shule ya Virginia Tech.
Rais Obama akielezea masikitiko yake kwa njia ya televisheni huku akipangusa machozi kila mara alisema pamoja nakutokea vitendo hivyo mara kwa mara lakini sasa juhudi zinahitajika ili kukomesha kabisa jambo hilo.
"Ninatoa rambirambi zangu kwa familia zote zilizokumbwa katika mkasa huu, najua mpo katika kipindi cha majonzi makubwa, ila nataka muelewe kuwa pamoja na urais wangu mimi pia ni mzazi, nimejeruhiwa kama jinsi walivyojeruhiwa wazazi wengine wa Amerika,"alisema
0 comments:
Post a Comment