Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO
VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 26/12/2012.
WILAYA YA MBEYA - MAUAJI
MNAMO TAREHE 25/12/2012
MAJIRA YA SAA 08:00HRS HUKO MAENEO YA SAE JIJI NA MKOA WA MBEYA, MTU
ASIYEFAHAMIKA JINA WALA ANUANI ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA 25-30,
MWENYE JINSIA YA KIUME ALIUAWA KWA KUKATWA NA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI
WAKE KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO NA KUMSABABISHIA KIFO CHAKE NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI TUHUMA ZA WIZI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWASAKA
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI BADALA YAKE WAWAFIKISHE WAHALIFU KWENYE MAMLAKA ZINAZOHUSIKA ILI
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA RUNGWE - MAUAJI
MNAMO TAREHE 25/12/2012 MAJIRA YA
SAA 06:00HRS HUKO MBEGELE KIJIJI CHA KAPYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA.
ITAMU S/O MWAKAGENDA, MIAKA 23, MNYAKYUSA NA MKAZI WA MWAKAGENDA ALIUAWA KWA
KUCHOMWA NA KISU KIFUANI UPANDE WA
KUSHOTO NA MTU AITWAYE NEBO D/O DAUDI @ ISALIKILA, MIAKA 21, MNYAKYUSA, MKULIMA
NA MKAZI WA MWAKAGENDA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KUGOMBANIA PANGA .MTUHUMIWA
ALITOROKA MARA BAADA YA TUKIO HILO JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA MTU/WATU MWENYE TAARIFA JUU YA SEHEMU ALIKO MTUHUMIWA HUYO AZITOE ILI
AKAMATWE NA KUFIKISHWA KWENYE MAMALAKA ZINAZOHUSIKA NA HATUA ZA SHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
WILAYA YA MBEYA - KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 25/12/2012 MAJIRA YA
SAA 11: 00HRS HUKO MWANJELWA JIJI NA MKOA WA MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA YESA S/O MWAKAPYELA,
MIAKA 21, MNYAKYUSA, NA MKAZI WA KABWE AKIWA NA KETE 5 ZA BHANGI. MBINU
ILIYOTUMIKA NI KUFICHA BHANGI HIYO MFUKONI KWA SURUALI YAKE. MTUHUMIWA NI
MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI .
WILAYA YA MBEYA - KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 25/12/2012 MAJIRA YA
SAA 11:45HRS HUKO MWANJELWA JIJI NA MKOA WA MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA
[1] VICTOR S/O NALALA, MIAKA 22,
MNDALI, NA MKAZI WA MAFIATI [2]
NSALA S/O MWACHUSYA, MIAKA 23, MNYAKLYUSA NA MKAZI WA MANGA NA [3] SABA S/O JUMA, MIAKA 19, ISLAMIC NA
MKAZI WA ILEMI WAKIWA NA KETE 34 ZA BHANGI. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUFICHA BHANGI
HIYO KATIKA MFUKO MWEUSI WA RAMBO. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WATUMIAJI WA BHANGI
WAPO MAHABUSU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA RUNGWE- KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 26/12/2012 MAJIRA YA
SAA 03:15HRS HUKO KITUO CHA POLISI TUKUYU WILAYA YA RUNGWE NA MKOA WA MBEYA
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA [1] FRANK S/O KYUSA, MIAKA 28, MNDALI,
MKULIMA, NA MKAZI WA BAGAMOYO AKIWA NA KETE 2 ZA BHANGI. MBINU ILIYOTUMIKA NI
KUFICHA BHANGI HIYO KATIKA MFUKO WA SURUALI YAKE BAADA YA KUPEKULIWA AKIWA
KITUONI KWA KOSA LA KUVUNJA NYUMBA TUK/IR/1517/2012
YAHUSIKA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI WA BHANGI YUPO MAHABUSU. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHANA NA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA - KUPATIKANA NA UNGA UNAODHANIWA KUWA NI DAWA ZA
KULEVYA
MNAMO TAREHE 25/12/2012 MAJIRA YA
SAA 11:56HRS HUKO MWANJELWA JIJI NA MKO WA MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA MERICK S/O SAMWEL, MIAKA 26, MNYAKYUSA, MKAZI WA MAFIATI AKIWA NA
UNGA UNAODHANIWA KUWA NI DAWA ZA KULEVYA MBINU ILIYOTUMIKA NI KUFICHA UNGA HUO
NDANI YA GANDA LA SIGARA . MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA UNGA HUO YUPO
MAHABUSU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA -KUPATIKANA NA
POMBE YA MOSHI
MNAMO TAREHE 25/12/2012 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO KINGANI UYOLE JIJI
NA MKOA WA MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA NEEMA D/O MAONI , MIAKA
26, MNYAKYUSA, MKAZI WA UYOLE [2]
DAUDI S/O MAHENGE, MIAKA 21, MKINGA, MKAZI WA SALAGA [3] WANGOLE S/O DANIEL, MNYAKYUSA, MIAKA 24, MKAZI WA GOMBE [4] RAPHAEL S/O MGAYA, MIAKA 22, MHEHE,
MKAZI WA UYOLE [5] JULIUS S/O
MASOKO, MSAFWA, MIAKA 25, MKAZI WA ITEZI NA [6] DIMONI S/O ADAMSON MIAKA 25,MKAZI WA IGAWILO WAKIWA NA POMBE YA
MOSHI LITA SITA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO WAPO MAHABUSU. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHANA NA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA - KUPATIKANA NA
POMBE YA MOSHI
MNAMO TAREHE 25/12/2012 MAJIRA YA
SAA 17:45HRS HUKO IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA AGNES D/O SANGA, MKINGA MKAZI WA KALOBE NA WENZAKE WANNE WAKIWA NA
POMBE MOSHI LITA KUMI [10] . WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA POMBE
HIYO WAPO MAHABUSU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU
YA MOSHI KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA.
WILAYA YA MBEYA - KUPATIKANA NA
POMBE YA MOSHI
MNAMO TAREHE 25/12/2012 MAJIRA YA
SAA 17:45HRS HUKO IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA LUTH D/O LUPASA , 48YRS , MNDALI NA
MKAZI WA IYUNGA AKIWA NA POMBE YA MOSHI LITA 08 . MTUHUMIWA NI MTUMIAJI
NA MUUZAJI WA POMBE HIYO YUPO MAHABUSU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI
NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA.
WILAYA YA MBEYA - KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI.
MNAMO TAREHE 25/12/2012 MAJIRA YA
SAA 12:50HRS HUKO UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA CHESCO S/O MBWILO, 20YRS MNYAKYUSA NA MKAZI WA HASANGA NA MICHAEL
S/O TILA, 21YRS MNYAKYUSA NA MKAZI WA MWANYANJE WAKIWA NA POMBE YA MOSHI LITA
03. MTUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO WAPO MAHABUSU. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHANA NA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA.
Signed By
[ DIWANI ATHUMANI -
ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
0 comments:
Post a Comment