Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitaka
maelezo zaidi kuhusu aina ya mbegu ya mahindi iliyotumika kutoka kwa Bi.
Grace Hokororo ambaye ni Bibishamba wa kata ya Itenka wakati alipokuwa
akikagua shamba darasa analolisimamia kwenye kijiji cha Itenka wilayani
Mlele, Katavi, jana jioni (Januari 6, 2013). Alifurahia kazi yake na
kuahidi kumpatia pikipiki imsaidie kutembelea vijijiji vingine vinne
anavyovisimamia.
Bibishamba wa kata ya Itenka, Bi.
Grace Hokororo akimshukuru Waziri Mkuu Mizengo kwa kufanya ukaguzi
kwenye shamba darasa analolisimamia analolisimamia katika kijiji cha
Itenka jana jioni (Januari 6, 2013) wilayani Mlele,
Katavi. Aliahidiwa kupatiwa pikipiki ili imsaidie kutembelea vijijiji
vingine vinne anavyovisimamia.
Bibishamba wa kata ya Itenka, Bi. Grace Hokororo akipokea zawadi ya sh. 305,000/- kutoka
kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambazo zilichangwa papo hapo na watu
alioandamana nao ili kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye shamba
darasa. Wa pili kulia ni Bw. Joseph Laurent anayesimamiwa na bibishamba
huyo ambaye shamba lake lilikaguliwa na Waziri Mkuu katika kijiji cha
Itenka jana jioni (Januari 6, 2013) wilayani Mlele,
Katavi. Pia aliahidiwa kupatiwa pikipiki ili imsaidie kutembelea
vijijiji vingine vinne anavyovisimamia.
0 comments:
Post a Comment