Pages

Home » » WAZIRI MKUU PINDA AZINDUA KITABU CHA WAPIMBWE

WAZIRI MKUU PINDA AZINDUA KITABU CHA WAPIMBWE

  
 *Ataka makabila mengine yatunze historia zao.
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua kitabu cha historia ya kabila la Wapimbwe lililoko mkoani Katavi na kutayataka makabila mengine kuandika historia zao ili waweze kutunza kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo.
 
Akizindua kitabu hicho hivi karibuni mjini Mpanda, Waziri Mkuu aliwataka watu wa makabila mengine ya mkoa wa Katavi ambayo ni Waruira, Wabende, Wakonongo na Warungwa wafanye tafiti kuhusu mila na tamaduni zao na kisha waandike vitabu vyao.
 
Kabla ya uzinduzi huo, mtunzi wa kitabu hicho, Bw. Peter Mgawe alisema kitabu hicho kimetokana na utafiti uliofanywa tangu mwaka 2007 ambao ulilenga kukusanya  taarifa na masimulizi mbalimbali kutoka kwa wazee wa Kipimbwe ambao wameishi miaka mingi huku wakiwa na hazina ya mila na tamaduni za kabila hilo ambalo pia ni kabila lake Waziri Mkuu Pinda.
 
“Hili ni kabila dogo lisilofahamika na wengi, nimekuwa nikitafuta taarifa na machapisho (literature) mbalimbali kuhusu kabila hili lakini sikuwahi kupata chochote… ndipo nikamshirikisha Mheshimiwa Waziri Mkuu juuya kufanya utafiti na kuandika historia yetu naye akalikubali wazo langu,” alisema Bw. Mgawe ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam.
 
Akizungumza na wakazi waliohudhuria uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema utafiti huo usiishie hapo tu, bali wafanye tafiti nyingine kuhusu mavazi, vyakula, ndege, wanyama waliokuwa wakipendelewa na mababu zao ili kuongeza hazina ya taarifa ya kabila hilo.
 
“Lengo la kitabu hiki lilikuwa ni kuhifadhi katika maandishi historia ambayo ilikuwa imefichika ndani ya vichwa vya wazee wetu kutoka vijiji mbalimbali vya Mpimbwe… nafurahi kwamba tunao wazee watatu waliokuwa katika warsha ya kwanza kabisa iliyofanyika mwaka 2008. Leo hii wako hapa na wanashuhudia matunda ya kazi yao,” alisema Waziri Mkuu.
 
Wazee hao ni Mzee Simba Pangani Kalulu (76) kutoka kijiji cha Mamba, Mzee Valeri Kipande (76)  kutoka kijiji cha Lyangalile na Mzee Moses Kasalani (67) kutoka kijiji cha Mirumba. Vijiji vyote hivyo viko wilaya ya Mlele, mkoani Katavi.
 
Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumanne, Januari 9, 2013) akitokea kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele, Katavi ambako alifanya ziara ya siku 10 kwenye jimbo lake la Katavi na kisha kuwa na mapumziko ya Krismasi na mwisho wa mwaka.
 
Wana nchi wa kata ya Itenka A jimbo la katavi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mh waziri mkuu Mizengo Pinda alipo kuwa ana hutubia kuhimiza watu kulima kwa kutumia kilimo cha kisasa mwishoni mwa wiki wana nchi wengine walilazimika kupanda juu ya miti (Picha na Chris Mfinanga)
 
Mke wa Waziri mkuu Mh Tunu Pinda akiwa ana sugua chungu ambacho hutumika katika ngoma marufu itwayo Nsimba  ya kabila la wapimbwe ambayo ilikuwa ikichezwa katika kata ya Itenka A na kikundi hicho  kinaitwa Pinda (Picha na Chris Mfinanga)
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger