Mgeni rasmi Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel (katikati) kwa
niaba ya Waziri Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara katika meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya Vijana
Kimataifa Duniani ambapo Tanzania iliadhimishwa katika viwanja vya
Temeke Mwembeyanga. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi. Mariam Khan
na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la AMREF Bw. Festus Ilako.
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi.
Mariam Khan (kushoto) akisalimia umati wa wakazi wa jijini Dar (hawapo
pichani) na kutoa ujumbe kwa vijana kuungana na kujiepusha na mangonjwa
hatarishi. Kulia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt.
Elisante Ole Gabriel.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel akiteta jambo na
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi. Mariam Khan.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana
Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha ujumbe kwa niaba ya
Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo ambapo amewataka vijana
kujitambua na kuwa na mikakati endelevu na kukaa kama vikundi ili
Serikali iweze kuwasaidia kupata misaada na kuwawezesha kuwa na
maendeleo endelevu katika siku hii ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa
ya Vijana Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 11 Agosti na kutimiza
malengo aliyokuwa akiyatafakari baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere juu
ya Vijana.
Umati wa wakazi wa Temeke katika
tamasha la siku ya maadhimisho ya Kimataifa ya Vijana Duniani ambako
zilifanyika shughuli mbambali ikiwemo Ujumbe kutoka Serikalini na Kupima
virusi vya Ukimwi bure.
0 comments:
Post a Comment