ANGELICA SULLUSI,Kyela,
WAANDISHI wa habari nchini
wametakiwa kujikita kwa kufuata madili ya taaluma kwa kutangaza na kuandika habari zenye tija kwa
jamii ambazo zinaleta uwiano sawa kwa jamii nzima hususani kwa habari za
wanawake.
Hayo yamesemwa na Mratibu
wa semina kwa waandishi wa habari za radio za jamii Rose Haji katika
semina ya siku saba kwa wanahabari iliyolenga
kuwajengea uwezo wa kutangaza na kuandika habari za kijamii iliyofanyika jana
Wilayani Kyela.
Amesema kuwa kwa kipindi
kirefu sasa wanawake wamekuwa hawasikiki kabisa katika vyombo vya habari wakati
na wao wana mambo mengi ya kuzungumzia.
Aidha,amesema kuwa
katika tafiti mbalimbali zilizofanywa kati ya mwaka 2003 na 2010 na
mpango unaoitwa Mahusiano ya Jinsia (gender links) kwa kushirikiana na MISA
ulibaini asilimia 17 ya vyombo vya habari vinatangaza habari za wanawake pekee.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa shirika la SIDA toka nchini
Sweeden ambao ni mradi wa miaka mitatu mfululizo kwa radio za jamii tisa nchini.
0 comments:
Post a Comment