Chama CHA RIADHA Mkoa wa Mbeya (MBERAA), kimefanikiwa kuteua
majina ya wanariadha 15 watakaouwakilisha mkoa huo kwenye mashindano ya taifa
yanayotarajiwa kufanyika Septemba saba Jijini Dar es salaam.
Akitangaza uteuzi huo muda mfupi baada ya kumalizika
mashindano ya mwisho ya mchujo yaliyofanyika katika uwanja wa kumbukumbu wa
Sokoine Jijini hapa, Katibu Msaidizi wa chama hicho mkoani hapa Moses Ng’wat,
alisema wachezaji hao ni wale waliofikia au kukaribia viwango vyas taifa kwa
kila kipengele.
Aliwataja waliochaguliwa katika mita 100 kwa upande wa
wanaume na wanawake na muda waliokimbia katika mabano kuwa ni Method Kahango (sekunde
12:00)na Watson Yatta (sekunde 12:08) kwa upande wa wanaume na wanawake ni
Elizabeth Mwakalobo (sekunde 14:02).
Aliwataja wengine katika mita 200 kuwa ni Peter Patrick (Sekunde
24:84),Watson Yatta (Sekunde 24:86)na Method Kahango (Sekunde 24:90) kwa upande
wa wanaume, na wanawake waliochaguliwa ni Elizabeth Mwakalobo (Sekunde 27:17)
na Nelly Issa (Sekunde 27:38).
Aliongeza kuwa waliochaguliwa katika mita 400 wanaume ni
Amos Mwakasya aliyekimbia sekunde 55:68, huku kwa upande wa wanawake
waliochaguliwa ni Mponjo Mwalyambi aliyekimbia Sekunde 59:95 na Anna Mwakalobo
aliyekimbia Sekunde 1:09.
Ng’wat aliwataja waliochaguliwa katika mbio za kati za mita 800 na 1500 kwa upande wa wanaume
na wanawake kuwa John Joel (Dakika
1:56:09), Bonface Andrew (Dakika 2:00) wanaume na wanawake ni bingwa wa taifa
wa mashindano ya shule za sekondari ,Maria Sikanyika aliyekimbia muda wa dakika
1;59:86.
Aliwatangaza wengine walioshinda na kuchaguliwa katika mita
500 kwa wanaume kuwa ni Moses Mwandemba alkiyekimbia kwa muda wa (dakika 15:45:62),
wakati katika kuruka chini waliochaguliwa ni Watson Yata aliyeruka (mita 6:20),
Christopher Jackson (Mita 6:10) na Bonface Andrew mita 5:95 kwa upoande wa
wanaume na Neema Kibonde (mita 4:30) kwa wanawake.
Hata hivyo kuhusu kambi katibu huyo Msaidizi alisema timu
hiyo inatarajia kuanza kambi Augost 22 mwaka huu na wachezaji hao watakuwa
chini ya mwalimu wa timu ya mkoa ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa
Tanzania Lwiza John, akisaidiwa na Jackob Ndawi.
Aidha, Ng’wat aliwataka wadau wa michezo katika ngazi zote
kujitokeza kuisaidia timu hiyo katika michango ya hali na mali ili iweze
kufanikiwa kujiandaa vizuri katika kipindi kilichobaki kabla ya kwenda kwenye
mashindano ya taifa Septemba saba mwaka huu jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment