









Mkuu wa
mkoa wa Iringa Dokta CHRISTINE ISHENGOMA amewataka wanahabari kulisaidia Taifa
katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuendelea kuhamasisha wananchi
kujitokeza katika zoezi hilo.
Mkuu huyo
wa mkoa ametoa Rai hiyo katika ukumbi wa Ruco mjini Iringa wakati wa ufunguzi
wa mafunzo ya siku mbili ya wanahabari kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini
pamoja na mkoa wa Lindi na Mtwara.
Alisema
kuwa zoezi hilo
la sensa ya watu na mkazi lina nafasi kubwa katika Taifa ili kuwezesha kupanga
bajeti kulingana na mahitaji sahihi ya wananchi wake.
Aidha
amesema kuwa sensa ya watu na makazi ni zoezi ambalo limekuwa likifanyika kila
baada ya miaka 10 hivyo lazima umma kujulishwa ili kujitokeza kwa wingi katika
zoezi Hilo.
Wakati
huohuo amewataka wakuu wa kaya kuweka kumbukumbu sahihi ambazo zitawezeshwa
makalani wa sensa kupata taarifa zilizo sahihi katika kufanikisha zoezi Hilo.
0 comments:
Post a Comment