Na Bosco Nyambege,Ileje-Mbeya
Jumla
ya wakazi 570 Wilayani Ileje Mkoani Mbeya wameunda kikundi
kitakachoweza kujenga mitambo ya kufua umeme katika maporomoko ya mto
Luswiswi katika Kijiji cha Bwenda yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya
megawati nane katika tarafa zaidi ya Bundali
Mitambo
hiyo ni mradi wa umeme Luswisi kikundi cha mazingira Ileje mashariki
ambao utaweza kusambaza katika kata 9 ambazo ni
lwiswisi,Lubanda,Ngulilo,Sange,Ngulungulu,Kafule,Ikinga,Malangali na
Ibaba.
Nia
kuu ya kuanzisha mradi huo ni kuweza kuwasaidia wananchi wa kata hiyo
ambao walikuwa wanatamani kupata nishati hiyo lakini hawakuweza kupata
nikutokana na Tanesco kutowafikishia umeme wakazi hao kwa wakati
muwafaka
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa mradi huo Lukasi Mtafya mpaka sasa mradi huo
unaendelea kuchunguzwa kwa kiwango kikubwa kwa kushirikiana na mradi
wa nishati ya umeme vijijini (Rural energing Agency)kupitia Benki ya
Dunia
Amesema kuwa katika hatua iliyofikiwa ni kupima kasi ya maji pamoja na usalama wa maji kwa matumizi ya binadamu
Hata
hivyo Mtafya amesema kuwa kikundi kinatarajia kukusanya shilingi
milioni36,Serikali inatarajia kuchangia kiasi cha shilingi miliono 146
na Halmashauri nya Wilaya ya Ileje inatarajia kuchangia kiasi chas
shilingi milioni 38.
Mtafya
amesema kuwa mradi huo utakapo kamilika wanatarajia kusambaza umeme
huo katika sehemu mbalimbali za makazin ya watu pamoja na sekta mbali
mbali za kiserikali
Kwa
upande wa wananchi waliopata wasaa wa kuzungumzia suala hilo wamesema
kuwa wanashukuru kwa wataalam hao kuweza kugungua maporomoko hayo
kwani ni muda mwingi walikuwa wanatamani kupata umeme lakini ilikuwa
wanpifgwa kalenda
Hivyo wameiomba serikali kuweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ili kuweza kufanikisha zoezi hilo kwa wakati mfupi.
0 comments:
Post a Comment