Na
Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Wajumbe
wa Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SARPCCO) wameanza kuwasili mjini
Zanzibar tayari kwa kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika
Septemba 5, mwaka huu.
Wajumbe
waliowasili leo ni pamoja na Mkuu wa INTERPOL. Kanda ya nchi za
Kusini mwa Afrika zilizopo Harare nchini Zimbabwe Bw. Chilika
Simfukwe, pamoja na maafisa wengine wa ofisi hiyo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP
Mussa Ali Mussa, amesma mkutano huo utafunguliwa na Makam wa wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Gharib Bilali.
Awali
Mkutano huo ulitarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano Dk. Jakaya Kikwete ambaye atakuwa na shughuli nyingine za
kitaifa.
Kamishna
Mussa amesema kuwa wengi wa wajumbe watakaowasili mjini Zanzibar ni
wale wa mikutano midogo midogo ya Kamati Tendaji za Wataalam wa
vitengo mbalimbali vya Majeshi ya Polisi kutoka nchi wanachama
mikutano ambayo itafanyika kuanzia Septemba 3 hadi 4, mwakahuu.
Amesema
kuwa mazimio yatakayofikiwa na kila kamati, yatafikishwa na
kuchambuliwa na Wakuu wa Majeshi ya Polisi katika mkutano wao
wa Septemba 5, mwaka huu.
Amesema
kuwa wakati wa mkutano huo, kutafanyika gwaride maalumu la kukabidhi
kitara kwa Mwenyekiti mpya wa Shirikisho hilo ambacho ni alama ya
uwenyekiti wa Shirikisho hilo.
0 comments:
Post a Comment