Na
Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Cat Work Agency imeandaa shoo ya mavazi iliyopewa jina la Green
Carpet Fashion Week ambayo pia itakuwa ni sehemu ya mchakato wa
kutafuta utambulisho wa vazi la taifa.
Mwanamitindo
na mratibu wa shoo hiyo, Gymkhana Hilal amesema kuwa shoo hiyo
itafanyika Desemba, mwaka huu kwenye Hoteli ya Giraffe iliyopo jijini
Dar es Salaam na itakuwa ni mwanzo wa utambulisho wa vazi la taifa
kwa kuwa baada ya hapo kutakuwa na mradi uliopewa jina la Jakaya
Project.
“Kutakuwa
na mavazi mbalimbali yatakayoonyeshwa siku hiyo, nipo kwenye
mazungumzo na makampuni kadhaa kwa ajili ya udhamini, lakini
wanamitindo wanaohitaji kushiriki wanaweza kufika katika ofisi zetu
zilizopo Kinondoni Biafra kwa ajili ya kujiandikisha au wanaweza
kupata maelezo zaidi kupitia tovuti yetu ya www.pakawear.com
“Mradi
wa Jakaya utakuwa umelenga kipindi cha runinga ambacho kitakuwa na
mwendelezo kwa kuwa kitakuwa kikirushwa kila wiki, unajua ni ngumu
kupata vazi moja liwe la taifa, lakini tunaweza kutengeneza mazingira
mazuri ya kuweka utambulisho wa vazi letu,” alisema Gymkhana.
Aliongeza
kuwa mpaka sasa ameshabuni mavazi kadhaa kwa ajili ya shoo hiyo
yakiwemo mavazi yaliyopewa jina la ‘Hip Hop Swahily style’, mbapo
ameanza mazungumzo na makampuni ya nguo ya hapa nchini ikiwa ni
sehemu ya kuthamini vitu vya nyumbani.
Gymkhana
aliongeza kuwa: “Tumeamua kuipa jina la Jakaya kwa kuwa rais wetu
wa sasa Jakaya Kikwete amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia vijana
na kuwafungulia njia katika mambo mengi, hivyo hii ni nafasi pekee
kwetu kuitumia kuonyesha uzalendo wetu.”
Gymkhana
amewahi kubuni mavazi katika amewahi kubuni mavazi katika shoo
mbalimbali zikiwemo Swahili Fashion Week, Khanga za Kale Fashion Show
na Lady In Red Fashion Show.
0 comments:
Post a Comment