Pages

Home » » ATOKOMEA KUSIKOJULIKANA BAADA YA KUMUUA MKEWE KWA KUTUMIA PANGA

ATOKOMEA KUSIKOJULIKANA BAADA YA KUMUUA MKEWE KWA KUTUMIA PANGA



Mkazi mmoja wa Kijiji cha Kogaja kata ya Goribe wilayani Rorya mkoani Mara Bw. Hamisi Omenda (33) amedaiwa kumuua kikatili mke wake Bi. Levina Hamisi (27)  kwa kumkatakata kwa panga na kisha kutoroka, huku Polisi wakidaiwa kushiriki katika utoro huo kwa kuandaa mazingira ya kutoroka.
Polisi wa kituo cha Kogaja wanadaiwa kuhusika na utoro huo kwa kile kilichodaiwa kuwa hawakumkamata mtuhumiwa licha kufika kituoni hapo kuchukua PF3 baada ya kufanya kitendo hicho.
Hata hivyo, taarifa kutoka Kituo cha Polisi Kogaja zimedai kuwa Mtuhumiwa ametoa maelezo kuwa mkewe  alikatwakatwa mapanga na watu wasiofahamika hivyo aliomba PF3 kwa ajili ya kumpeleka marehemu katika  Hospitali ya Tarime mjini Tarime.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji wa Kijiji cha Kogaja, Bw. Lukas Ambonya amekiri Bw. Omenda kuhusika katika tukio hilo na kwamba wakiwa njiani kwenda hospitalini  mke wake alifariki na yeye kutokomea kusikojulikana hivyo hakuwepo hata wakati wa maziko.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger