Pages

Home » » DAR KWACHAFUKA, VURUGU ZATANDA KATI YA POLISI NA WAISLAM

DAR KWACHAFUKA, VURUGU ZATANDA KATI YA POLISI NA WAISLAM



Waislamu Jijini Dar es salaam wamefanya maandamo yenye lengo la kushinikiza kiongozi wao kupewa dhamana mahakamani licha ya maandamano hayo kupingwa na Serikali.
Kutokana na maandamano hayo jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam imelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waumini hao wa dini ya kiislamu walioonekana kuzagaa katika maeneo ya jiji hilo wakifanya maandamano.
Awali kabla ya kufanyika kwa maandamano hayo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam SADICK MECK SADIC alikutana na viongozi wa dini hiyo na kukubaliana kutofanyika kwa maandamano hayo.
Hata hivyo waislamu hao wameonekana kukaidi agizo hilo na hivyo kuingia barabarani mara baada ya kumaliza ibada yao ya Ijumaa.
Kwa habari zaidi kuhusu vurugu za huko jijini Dar es salaam tutaendelea kuwafahamisha kupitia vipindi vyetu vijavyo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger