Pages

Home » » MWANAJESHI MMOJA AFA KWA AJAL YA NDEGE DAR

MWANAJESHI MMOJA AFA KWA AJAL YA NDEGE DAR

Mwanajeshi mmoja amefariki  dunia na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya ndege waliokuwa wakiirusha kuanguka leo jijini Dar es Salaam.
Ndege hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWT) ilikuwa na marubani wawili na mmoja alifariki dunia wakati akijaribu kuruka baada ya  ndege hiyo kupata hitilafu
wakati ikiwa hewani karibu na eneo hilo.
Tukio hilo limetokea leo katika kambi ya Jeshi la Anga, Ukonga jijini Dar es Salaam. Mwili wa mwanajeshi aliyefariki umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi ya  Lugalo, Dar es Salaam.
Askari aliyejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo ni Kapteni Feruz Kwibika ambaye alipasuka kichwa na kulazwa katika hospitali hiyo. Kwibika alijeruhiwa vibaya baada  ya kuruka kutoka ndani ya ndege hiyo kwa lengo la kuokoa maisha yake baada ya kutokea hitilafu hiyo.
Wanajeshi hao walikuwa kwenye mafunzo ya kawaida ambayo JWT wamekuwa wakifanya kwa ajili ya kuwajenga vijana wa jeshi hilo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger