Pages

Home » » Sofia Simba Ashinda Tena UWT

Sofia Simba Ashinda Tena UWT


Leo Dodoma
Bilal Afungua Mkutano Wa UWT Taifa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika leo Oktoba 20, 2012 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma leo Oktoba 20, 2012 kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania, (UWT) Taifa, anayemaliza muda wake, Sophia Simba, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika leo Oktoba 20, 2012, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa.
 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, anayemaliza muda wake, Sophia Simba (katikati) na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika leo Oktoba 20, 2012, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT waliohudhuria mkutano huo leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
 
 
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger