Pages

Home » » BalozI Peter Kallaghe Akutana Na Maafisa Wa Bodi Ya Utalii TTB

BalozI Peter Kallaghe Akutana Na Maafisa Wa Bodi Ya Utalii TTB

Mh.Balozi wa Tanzania nchini Uingereza  Balozi Peter Kallaghe leo ameitisha mkutano kati yake na maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na maafisa wa Ubalozi ili kuzungumza nao na  kupata taarifa muhimu  juu ya maadandalizi ya ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya utalii ya (WTM),  yanayotarajiwa kuanza siku ya jumatatu Novema 5 mpaka Novemba 8 mwaka huu katika jiji la London.
Maonyesho ya Utalii ya (WTM)  yanayoandaliwa nchini Uingereza ni maonyesho makubwa  na yanashirikisha makampuni kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa ajili ya kuuza bidhaa zao, hasa Mahoteli, Makampuni ya Ndege na makampuni ya Utalii, Mwaka huu Tanzania inashirikisha makampuni zaidi ya 55 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Katika picha juu akisisitiza jambo katika mkutano huo, wakati wa mkutano huo ambapo aliza kila jambo ambalo linahitaji kupata majwabu muhimu kabla ya kuanza kwa maonyesho hayo.
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akifafanua jambo katika mkutano huo, kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi.

 Maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wakimsikiliza kwa makini Mh. Balozi Peter Kallaghe wakati akiongea nao katika mkutano huo
Balozi Peter Kallaghe akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Ubalozi na Bodi ya Utalii Tanzania TTB katika ubalozi huo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger