Meneja wa Baraza la Habari kanda ya Zanzibar (MCT) Suleiman Seif Omar
akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu tamko la
Tume ya utangazaji Zanzibar kupiga marufuku kuripoti taarifa za UAMSHO
zenye kuashiria uvunjifu amani kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT
John P.Mireny
Kaimu Katibu Mtendaji wa (MCT)John P.Mireny akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa Habari hawapo pichani juu yatamko la Tume ya utangazaji
Zanzibar kukifungia chombo cha TVna Radio. Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifatilia kwa makini juu ya ufafanuzi
uliotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT John P.Mireny huko katika
ukumbi wa MCT uliopo Mlandege mjini Zanzibar
Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT John P.Mireny akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari juu ya tamko la Tume ya utangazaji Zanzibar kukifungia chombo cha TVna Radio iwapo kitaripoti habari za UAMSHO zenyekuashiria ufunjifu wa amani .
Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT John P.Mireny akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari juu ya tamko la Tume ya utangazaji Zanzibar kukifungia chombo cha TVna Radio iwapo kitaripoti habari za UAMSHO zenyekuashiria ufunjifu wa amani .
BARAZA LA HABARI TANZANIA MCT LIMESEMA
KUWA LIMESHTUSHWA TAARIFA YAKUZUIWA KWA VYOMBO VYA HABARI VYA ZANZIBAR
KUTANGAZA KHABARI ZINAZOHUSIANA NA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA
YAKIISLAM ZANZIBAR.
HAYO YAMEELEZWA JANA NA KAIMU KATIBU
MTENDAJI WA BARAZA HILO NDUGU JOHN MIRENYI WAKATI AKIZUNGUMZA NA
WAANDISHI WA KHABARI KATIKA UKUMBI WA MCT MLANDEGE MJINI ZANZIBAR.
BARAZA HILO LIMEONGEZA KUWA LINAAMINI KUWA SI VIZURI KUINGILIAA UHURU WA VYOMBO VYA KHABARI NA WAHARIRI.
AIDHA MIRENYI AMEVITAKA VYOMBO VYA
KHABARI VYA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR KUFANYA KAZI ZAKE BILA YA
WOGA,UPENDELEO NAKUZINGATIA MAADILI NA KANUNI ZINAZOONGOZA UANDISHI WA
KHABARI.
AMESISITIZA KUWA LICHA YA BARAZA LA
KHABARI TANZANIA KUTAMBUA NAKUTETEA KWA NGUVU ZOTE KUWEPO KWA UHURU WA
VYOMBO VYA KHABARI NAKUJIELEZA VYOMBO VYA KHABARI VINA WAJIBU
WAKUJIEPUSHA KURIPOTI KHABARI ZA UCHOCHEZI WOWOTE UNAOWEZA KUHAMASISHA
CHUKI KWA JAMII NA HATIMAYE KUVURUGA AMANI YA NCHI.
TAMKO HILO LA MCT LIMEKUJA KUFUATIA
HATUA YA HIVI KARIBUNI YA TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR KUPIGA MARUFUKU
MATANGAZO YOTE YANAYOHUSIANA NA VURUGU ZINAZOHUSISHWA NA JUMUIYA YA
UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR KWA VITUO VYOTE VYA RADIO NA
TELEVISHENI BINAFSI HAPA NCHINI.
KIONGOZI HUYO AMEELEZEA HAJA KWA VYOMBO VYA KHABARI KUZINGATIA UWAJIBIKAJI NA KUWA MAKINI ILI KUEPUKA KUCHOCHEA VURUGU
0 comments:
Post a Comment