Watu wasiopungua 10
wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa baada ya treni mbili kugongana huko kusini
magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Imearifiwa kuwa treni moja ilikuwa
ikitoka mji mkuu Kinshasa na ya pili kutoka Matadi mji mkuu wa mkoa wa
Bas-Congo wakati ajali hiyo ilipojiri Jumamosi katika eneo la Songololo
karibu na Matadi.
Sababu ya ajali hiyo haijulikani lakini
uharibifu mkubwa umeripotiwa kutokea baad aya treni hizo kugongana. Reli ya
Matadi-Kinshasa yenye urefu wa kilomita 365 ilianza kutumiwa mwaka 1898 na
imechakaa kabisa.
Ajali za treni hutokea mara kwa mara
Kongo kutokana na ukosefu wa ukarabati wa reli zilizojengwa wakati wa ukoloni.
0 comments:
Post a Comment