MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi Taifa ameibua tuhuma nzito na kusema kuwa kuna mpango mchafu
unaosukwa kwa lengo la kuhakikisha Mwenyekiti wa Taifa Rais Jakaya Kikwete
anang’olewa nafasi hiyo kwa kupigiwa kura za hapana.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dodoma jana, Mjumbe huyo Agustino Matefu alisema kuwa
wamegundua baadhi ya vipeperushi ambavyo vitasambazwa siku moja kabla ya
uchaguzi na kuwataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kutounga mkono uchafu huo
na uhuni unaoongozwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi.
Mmoja
wa vipeperushi hivyo ambavyo gazeti hili lina nakala yake kilikuwa Kimeandikwa:
“Ndugu Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Chama chetu kinayumba eti kwa pamoja
tumpunguzie mzigo mheshimiwa Rais kwa kumvua kofia moja ya Uenyekiti, kwa
pamoja tutashinda piga kura ya hapana kwake,” kilisema moja ya kipeperushi
hicho chenye nembo ya Chama Cha Mapinduzi.
Alisema
kuwa moja ya vipeperushi hivyo kilikutwa Dodoma Hotel ambapo Hussein Bashe na
wenzake watatu walipokuwa kwenye kikao usiku wa kuamkia jana na walifika hapo
baada ya kupata taarifa ya kikao hicho na kufuatilia.
Aliwataja
wengine hao kuwa Beno Malisa, Martine Shigela na Fred Lowassa. Alipohojiwa
Bashe alikanusha kuhusika na kampeni za kumng’oa Kikwete wala vipeperushi hivyo
na kusema kuwa hizo ni fitina za kisiasa.
Mjumbe
huyo wa mkutano mkuu alisema kuwa, mafisadi wametenga jumla ya shilingi bilioni
tano kwa lengo la kupitisha wajumbe wao wa NEC ambao watasimamia maslahi yao ya
Urais.
Alisema
kuwa kuna haja ya kukataa na kupinga mipango michafu kama hiyo yenye lengo la
kukifedhehesha chama na kukitia aibu na kuonekana kuwa ni chama cha watu
fulani.
Mjumbe
huyo wa mkutano mkuu alisema kuwa yuko tayari kutoa ushahidi kutokana na hayo
anayoongea kwani ana ushahidi nayo
Chanzo.Jaizmela leo.
0 comments:
Post a Comment