Mkurugenzi
wa Shirika la Upelelezi la Marekani CIA, David Patreaus amejiuzulu hapo jana
kutokana na kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa ambayo yamezua hali isiyofaa kwake
kuendelea na kazi hiyo.
Petreus,
ambaye alichukua wadhifa huo miezi 14 iliyopita baada ya kustaafu katika jeshi
la Marekani akiwa Jenerali mwenye nyota nne amefafanua kuhusu uamuzi wake huo
katika barua yaliyoiandika kwa maafisa wa shirika hilo jana Ijumaa ( 09.11.2012).
Katika
barua hiyo Petraeus ameandika akisema "baada ya kuishi katika maisha ya
ndoa kwa miaka 37, nimeonyesha udhaifu kwa kujihusisha na mahusiano mengine nje
ya ndoa hiyo. Tabia hiyo haikubaliki kote, kama mume na pia kama kiongozi wa
taasisi kama hii yetu. Mchana huu, rais (Obama) amekubali ombi langu la
kujiuzulu."
Hata
hivyo hakukuwa na taarifa rasmi juu ya lini mahusiano hayo yalifanyika na nani
alihusika. Mwandishi wa mtandao wa Slate.com Fred Kaplan, ambaye amewahi
kuandika kuhusu Patraeus na ushawishi alionao katika mipango ya jeshi la
Marekani amekiambia kituo cha televisheni cha CNN kuwa kiongozi huyo alikuwa na
mahusiano na mwandishi Paula Broadwell.
Broadwell
alitumia mwaka mmoja kumfuata Petraeus nchini Afghanistan kabla ya kuandika
wasifu wake 2012 uliopewa jina la "All in: The education of General
Petraeus." Picha yake katika mtandao wa Amazon.com inamuonyesha akiwa
amekaa karibu na mahali alipokaa Patreaus huku ujumbe wake wa mwisho katika
mtandao wa Twitter siku ya Jumatatu unahusu uongozi wa falsafa ya Maxim wa
Jenerali huyo.
Amesema
kuwa sababu za kujiuzulu kwake ni za binafsi zaidi na hazihusiki na uchunguzi
unaoendelea kuhusu uvamizi wa ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi, Libya,
ambako Balozi wa Marekani na maafisa wengine waliuawa.
CNN
inaripoti kuwa Shirika la Ujasusi la Marekani, FBI, linachunguza iwapo uamuzi
huo ulitokana na hatari za kiusalama ikiwa ni pamoja na kujua kama Petraeus
inawezekana kuwa alitishwa kutokana na mahusiano yake hayo.
Mahusiano
ya nje ya ndoa ni suala nyeti katika tasnia ya usalama. Mahusiano hayo yanaweza
kuwa kitisho kwa taaluma hasa kwa maafisa wanaoshikilia nafasi za juu kwenye
majeshi na taasisi za usalama.
Mbinu
za jenerali huyo aliyepata sifa tele zimesaidia kuharakisha kuondolewa kwa
jeshi la Marekani nchini Iraq. Alikuwa kamanda wa vita vya Afghanistan kabla ya
kushika wadhifa huo wa mkuu wa CIA.
Petraeus
mwenye umri wa miaka 60 alistaafu jeshi akiwa Jenerali mwenye nyota tano na
muda mfupi baadae alipewa wadhifa huo wa kuiongoza CIA. Ni mhitimu wa Chuo
Kikuu cha kijeshi cha Marekani katika eneo la West Point mjini New York pamoja
na Chuo Kikuu cha Princeton.
0 comments:
Post a Comment