*Binti huyo yadaiwa ni Mke wake.
*Mchungaji huyo atoa sh. 20,000/= ili binti aitoe mimba hiyo.
*Askofu afuatilia sakata hilo.
Na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Mchungaji
wa Kanisa la Reedemed Gospel Church John Mgalah(38) lililopo Kijiji cha
Namlonga, Kata ya Ruanda, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya, anadaiwa kumpa
mimba muumini wake Mariam Mwakabata(18), Mkazi wa Kijiji cha Idibila
Wilayani humo.
Tukio
hili ni kufuatia muumini huyo kudai alipigiwa simu na mchungaji huyo
mnamo Selida Mtafya mwenye watoto sita akiwa amekwenda wilaya ya Mbeya
katika Hospitali ya Ifisi kupatiwa matibabu.
Mariam
amedai kuwa aliwasili kijijini hapo akitokea Mji mdogo wa Tunduma,
alipokuwa amekwenda kuwasalimu kaka zake majira ya saa 11 wakati
mchungaji akishiriki harusi ya Bwana Mika Msolina iliyokuwa ikifungwa
kanisani hilo.
Aidha
binti huyo amedai kuwa mchungaji alimtaka kutangulia nyumbani kwake
naye kuitikia wito wa mchungaji, ambapo aliwasili saa 3:00 usiku na
mchungaji kuwasili majira ya saa 4:00 usiku na kumtaka binti aende
nyumba ya nje na kisha kukubali na mara baada ya mchungaji kufika
alianza kumtomasasehemu mbalimbali, hali ambayo ilimfanya binti huyo
kupiga kelele na mchungaji kutoka nje.
Mchungaji alirejea mara ya pili ndani ndipo alipofanikiwa kumbaka na kumsababishia ujauzito sasa ni miezi mitatu.
Baada
ya kupitia mwezi mmoja kupita Binti huyo alimpigia simu mchungaji na
kumueleza hali halisi ambapo alimtaka binti huyo kuitoa mimba na kumpa
shilingi 20,000, lakini Mariam alipokea pesa hizo lakini hakwenda kuitoa
mimba hiyo.
Binti
huyo alianza kuutaarifa uongozi wa kanisa kufuatia mimba hiyo hiyo
ndopo mchungaji alianza na yeye kukamilisha mchungaji alianza naye
kukamilisha kumpa ujauzito huo.
Kwa
upande wake Mchungaji alikanusha kuhusika na tendo hilo na kwamba binti
uyo ana nia ya kumchafua tu ingawa binti huyo kulala kwake siku hiyo ya
harusi na kudai alikuwa na ugomvi wa na familia yake.
Hata
hivyo Askofu wa Kanisa hilo, Tawi la Mlowo wilayani humo Anyimike
Mwaitumile amekiri kupokea shauri hilo na kwamba wanafanya uchunguzi na
pindi atakapobainika watamchukulia hatua za kinidhamu kwa mtumishi huyo
na kwamba wachungaji wa kanisa hilo wanatakiwa kujiepusha na mabinti
kwani wanaweza kuwatondosha katika imani.
Wakati
huo huo Serikali ya Kitongoji kupitia Bwana Asaulile Mwakimwili
amesema kuwa suala hilo lipo kwenye Ofisi yake na wameweza kukutana na
pande zote mbili na Mchungaji kukanusha lakini suala hilo likiwa
limefikishwa katika Ofisi ya serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti wa
Kijiji Bwana Asavule Mwakimwile na Afisa Mtendaji wa kijiji Bwana Beck T
Siwale na kudai kuwa wanachosubiri barua ili sheria iweze kuchukua
mkondo wake.
0 comments:
Post a Comment