Picha hii haiendani na picha tukio lakini picha hii pia wananchi walikuwa wakifanya uokoaji baada ya kijana mmoja kudumbikia chooni na kufa papo hapo.
Na.Gabriel Mbwille, Mbozi
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la TIENA
MWAZEMBE mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji Hangomba kata ya Bara wilayani
Mbozi mkoani Mbeya amenusurika kufa
baada ya kutumbukia chooni wakati akifanya mapenzi huku memewe akiwa mahututi
chumbani.
Habari
za uhakika kutoka kijiji hapo zinadai kuwa mwanamke huyo licha ya kuwa mke wa
mtu alikuwa anafanya ngono chooni na WASI MGALA wakati mumewe akiwa ndani
anaumwa na kwamba alidumbukia choo baada ya banzi alilokuwa amekanyaga kukatika
wakati wanafanya tendo hilo.
Mwanamke
huyo alidumbikia kwenye choo chenye urefu wa futi 17 na kwamba baada ya kudumbukia,
mwanaume aliyekuwa naye chooni wakifanya ngono alikimbia na kumwancha mwanamke
huyo akipiga kelele za kuomba msaada ndipo wananchi walifika na kufanikiwa
kumtoa ndani ya shimo na kukimbiza kwenye dula la madwa linalomilikiwa na
muuguzi LEONARD NZOWA ambaye alitoa huduma ya kwanza kabla ya kumfika katika
hospitali ya Mbozi Mission.
Hata
hivyo mume wa mwanamke huyo SAIKI GODFREY KAROTI amesema kitendo kilichofanywa
na mkewe ni cha uzalilishaji na si cha uungwana.
CTRL + Q to Enable/Disable GoPhoto.it
0 comments:
Post a Comment