Leo Ni Siku Ya Kuamua Kwa Wamarekani
MAREKANI
Ripoti mpya zinaonyesha kuwa mamilioni ya Wamarekani wameamua
kutopiga kura katika uchaguzi wa 57 wa Rais nchini humo.
Ripoti zilizotolewa jana zinaonyesha kuwa jumla ya raia
milioni 90 waliotimisha masharti ya kupiga kura hawatashiriki katika
uchaguzi huo na kwamba ni watu milioni 150 pekee ndio waliojiandikisha kupiga
kura kati ya milioni 207 waliotimiza masharti ya kupiga kura huko Marekani.
Uchunguzi wa maoni uliofanywa pia na taasisi ya Gallup kuanzia Oktoba 15
hadi 28 unaonyesha kuwa ushiriki wa watu katika uchaguzi wa Rais wa mwaka huu
huko Marekani utakuwa wa chini ikilinganishwa na ule uliofanyika katika chaguzi
mbili zilizotangulia.
Wakati huo huo Rais Barack Obama wa Marekani amewataka
wafuasi wake wawashawishi ndugu na marafiki zao washiriki kwenye uchaguzi wa
rais wa Jumanne ya leo.
Akizungumza jana usiku mbele ya hadhara ya wafuasi wake,
Obama alisema na hapa ninamnukuu" hili ni jukumula kila raia wa Marekani
kushiriki katika uchaguzi", mwisho wa kunukuu.
Amesema chama cha Democrat kitashinda pia katika
uchaguzi huu wa leo kama kilivyoshinda katika
uchaguzi wa mwaka 2008.
0 comments:
Post a Comment