Serikali ya Uganda imeazimia kuvitoa
vikosi vyake nchini Somalia. Patrick Amama Mbabazi Waziri Mkuu wa
Uganda ameliambia bunge la nchi hiyo na kuongeza kuwa, hatua hiyo
imechukuliwa ikiwa ni radiamali kutokana na tuhuma zilizotolewa na Umoja
wa Mataifa kwamba nchi hiyo inawasaidia zana za kivita waasi wa March
23 wanaopambana na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Amama
Mbabazi ameongeza kuwa, katika hali ambayo wanajeshi wa Uganda chini ya
mwamvuli wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika wako nchini
Somalia na baadhi yao wamepoteza maisha yao kwa shabaha ya kupambana na
makundi ya waasi nchini humo, huku Umoja wa Mataifa unadiriki kutoa
madai na tuhuma zisizo na msingi kwamba Kampala inawasaidia zana za
kijeshi waasi wa March 23.
Timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa
ilitayarisha ripoti ya kurasa 44 na kuzituhumu nchi za Rwanda na Uganda
kwa kukiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa kwa kuwapelekea silaha kwa
waasi wa kundi la M23.
0 comments:
Post a Comment