UGANDA 2 KENYA 1!
ZANZIBAR yatwaa Dola 10,000 kwa Matuta!!
Kwenye Fainali, Uganda walitangulia kupata Bao katika Dakika ya 28 baada ya Anthony Kimani kujifunga mwenyewe na Kenya waliweza kusawazisha katka Dakika ya 87 kwa Bao la Edwin Lavasta lakini Uganda wakaunyaka Ubingwa katika Dakika ya 90 kwa Bao la Geofrey ‘Baba’ Kizito.
Katka Mechi ya kusaka Mshindi wa Tatu, Zanzibar Heroes iliwabwaga Kilimanjaro Stars kwa Penati 6-5 baada ya kwenda sare 1-1 katika Dakika 90 za mchezo.
Stars ndio walitangulia kufunga kwa Bao la Mwinyi Kazimoto katika Dakika ya 20 na Zanzibar kusawazisha kwa Bao la Othman Ally zikiwa zimebaki Dakika 5.
Ndipo zikaja Penati tano tano na Zanzibar kushinda kwa Penati 6-5.
VIKOSI:
KILI STARS: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Amri Kiemba, Athman Idd, Shaban Musa, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngasa, John Bosco
ZANZIBAR: Abdalla Rashid Abdalla, Nadir Cannavaro, Nassor Masoud Said, Samih Nuhu Haji, Aggrey Ambrose Morris, Sabri Alliy Makame, Suleyman Kassim Suleyman, Khamis Mcha Khamis, Jaku Juma Jaku, Seif Rashid Abdalla, Abdulghan Gulam Abdalla
MATOKEO:
MSHINDI wa TATU:
Zanzibar 1 Kili Stars 1 [Zanzibar yashinda Penati 6-5]
FAINALI: Desemba 8
Uganda 2 Kenya 1
0 comments:
Post a Comment