Pages

Home » » KIKWETE KUONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA BARA

KIKWETE KUONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA BARA

GWARIDE LA MAJARIBIO LA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA

Kikosi cha Gwaride cha Jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ) Kikipita  mbele ya maofisa wa Vyombo vya ulinzi na Usalama wakati wa gwaride la majaribio  la kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania katika uwanja wa Uhuru leo asubuhi ambapo keshokutwa Desema 9 mwaka huu maadhimisho hayo yatafanyika katika uwanja huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kikosi cha jeshi la Magereza kikipita mbele ya maofisa hao
Kikosi cha Bendera kutoka Jeshi la Wananchi la Tanzania JWTZ kikipita.
Kikosi cha Wanamaji kikitembea kwa Mwendo wa Polepole.
………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 Dar es salaam
 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amewaomba wakazi wa jiji la Dar es salaam  kujitokeza kwa wingi kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika zitakazofanyika katika Uwanja wa Uhuru jiji Dar es salaam.

 
Akitoa ufafanuzi wa kukamilika kwa maandalizi ya sherehe hizo leo  jijini Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na mwaka huu  mkoa wa Dar es salaam umepewa heshima ya kuandaa sherehe za kutimiza miaka 51 ya uhuru.
 
Amesema  katika kipindi cha miaka 51 ya uhuru Tanzania imepata mafanikio makubwa  katika nyanja mbalimbali  za uchumi, ulinzi na usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa.
 
Amefafanua  kuwa  mgeni rasmi katika maadhimisho  hayo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete na kuongeza  kuwa yataongozwa na kauli mbiu isemayo  Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu.
 
Aidha amefafanua kuwa sherehe za mwaka huu zitahudhuriwa na ugeni wa marais kutoka Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na kupambwa na gwaride maalum lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania , halaiki maalum, vikundi mbalimbali vya burudani vya ngoma za asili vya hapa Tanzania  hususani kutoka maeneo ya Ukerewe, Dodoma na Zanzibar.
 
Vikundi vingine vitakavyopamba sherehe hizo ni kundi la Taifa la sanaa kutoka nchini Rwanda (Rwanda National Ballet).
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger