Pages

Home » » Chris Lukosi; " Kwa nini Nimeondoka Chadema..."

Chris Lukosi; " Kwa nini Nimeondoka Chadema..."


Leo hii nimeamua rasmi kurudi CCM, chama ambacho nimekifahamu kwa miaka 35 sasa.

  Nilijiunga na Chadema kwa matumaini niliyokuwa nayo kuwa ni chama kitakachomkomboa Mtanzania kutoka kwenye umasikini na kumfikisha kwenye level sawa na watu wa mataifa mengine kama Botswana , Namibia au hata baadhi ya nchi za Ulaya.

Niliamua haya baada ya kufuatilia yanayoandikwa kwenye vyombo vya habari kwa sababu mie binafsi kwa sasa naishi UK hivyo basi mambo mengi yatokeayo nyumbani huwa nayapata kwa kusoma magazeti na blogs mbali mbali.

Nilifanikiwa kukutana na Mheshimiwa Lema hapa London ambapo tukapanga mikakati ya kukijenga chama hapa UK na nikapewa jukumu la kufungua matawi nchi nzima na kuhamasisha Watanzania, kazi ambayo niliifanya kwa moyo mmoja. Pia nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chadema UK.

Nimefanikiwa kuhamasisha watu wengi na baada ya miezi michache niliamua kwenda nyumbani kuona hali ilivyo. Niliyoyakuta ilikuwa tofauti na niliyokuwa nikiyasikia na kusoma.

NIMEKUTA BARABARA NZURI SIJAWAHI KUONA TOKA NIZALIWE NA ZINAENDELA KUJENGWA!

SHULE ZA SEKONDARI KILA KATA NA VYUO VIKUU VYA KUJICHAGULIA.

MAISHA YA WATANZANIA YAMEBADILIKA SANA - MIDDLE CLASS NI MAISHA YA KAWAIDA TU. VIJANA WENGI WAMEENDELEA TOFAUTI NA ZAMANI MPAKA UWE MCHAWI KIDOGO NDIO UWE TAJIRI. MIJI INAJENGEKA KWA KASI YA AJABU. UKIHARIBU KAZINI UTAWAJIBIKA .

 Na mengine mengi tu niliyaona mpaka nikaanza kujiuliza , hivi najiita mpinzani, NINAPINGA NINI?

 Kama ni maendeleo nayaona tena maendelo original Nikakumbuka msemo mmoja... “KWA NINI UHANGAIKE NA FOTOKOPI WAKATI ORIGINAL IPOO?”

Kwangu mimi CCM ni original na Chadema ni photocopy, tena copy iliyotolewa wakati mashine imekwisha wino . Mabadiliko ya kweli yatatokea ndani ya CCM na si kwingineko!

 Kuna mengi mazito yamenichefua Chadema lakini sitayasema leo. Juzi mwenyekiti wangu wa Taifa Mheshimiwa Mbowe alipita hapa UK, lakini, mpaka ameondoka hakutaka kuwasiliana na kiongozi yoyote wa Chadema hapa UK kitendo ambacho kiliniuma sana, kwani, niliona kama tumedharauliwa;

  BABA HUWEZI KWENDA SEHEMU WALIPO WANAO UKASHINDWA HATA KUWAPIGIA SIMU KUWAJULIA HALI.

Ni matumaini yangu kuwa uamuzi wangu utaeleweka. Kama tujuavyo, kila kwenye msafara wa mamba na kenge wamo, lakini naona kwenye msafara wa Chadema idadi ya kenge inazidi mamba.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger